CHAPATI HIZI NI SAFI KABISA KWA FAMILIA KUBWA KUTOPIKA MARA KWA MARA UNAPIKA NYINGI NA UNAZITUNZA WIKI MOJA NA ZIKABAKI NA UBORA ULEULE, PIA NYAMA HII YA MBUZI INAKUA HAINA HARUFU MTU YEYOTE ANAWEZA KULA KWA AINA HII YA MAPISHI NA AKAFURAHIA SANA
MAHITAJI
1 kg unga wa ngano
1 kikombe kimoja
1 kijiko kidogo cha chai chumvi
nusu kikombeha chai mafuta ya kupikia
2 mayai kuongeza ladha
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEKEZO CHINI
unga wa ngano
Weka mafuta katika unga
kisha weka moto sana katika unga
kisha changanya kwa kutumia mwiko maana maji ni yamoto sana
weka chumvi
kishaanza kukanda kwa mkono maji yatakua yameshapoa
kanda unga safi kabisa uchanganyike
kisha anza kusukuma unga wote
baad ya hapo mwagia kwa juu mafuta ya kula pakaza eneo lote
hakikisha mafuta yameenea unga wote
kisha kunja pole pole unga wote kutengeneza mduara
kisha kata maumbo madogo ya usawa kwa kutumia kisu
baada ya hapo chuku yale maumbo uliyokata geuza na uyakandamize safi mpka chini
hapa ni baada ya kuzikandamiza
kisha chukua mti wa kusukumia na zisukume mapak upate upana wa kawaida tayari kwa kuzichoma
weka katika kikaango kikavu kisha zungusha chapati hiyo kw kutumia mkono
iache kidogo ichomwe
kisha igeuze baada ya kuiva upande mmoja
ikandamize tena kwa upande wa pili bado ikiwa kavu bila mafuta kama ni yamoto sana basi tumia karatasi kukandamizia
weka mafuta ya kupikia kwa juu hakikisha unasambaza chapati yote ienee
kisha geuza a upande wa pili paka pia mafuta
Toa weka katika sahani itakua imeiva safi kabisa tayari wa kuliwa
weka pembeni zipoe kisha unaziwekakatika sahani unatumbukiza katik mfuko wa plastiki usiweke kwenye friji weka tu nje zitakua safi na laini zinakaa wiki 1 baada ya hapo zitapoteza ubora ukitaka kula unatoa unapasha kwenye kikaango au kwenye micro wave inakua yamoto na laini zaidi na iliyochambuka kwa ubora uleule
MAHITAJI NYAMA YA MBUZI
1 kilo nyama ya mbuzi
1 kitunguu kikubwa
1 nyanya ya kopo
1 kijiko kidogo cha chai kitunguu swaumu
3 viazi ulaya
1 kikombe kilichojaa mchanganyiko w mboga majani
1 kikombe cha maji baridi
1/2 kikombe mafuta ya kupikia
weka mafuta katika sufuri yakishapata moto weka kitunguu maji kaanga
hii ni nyama ya mbuzi ya mifupa inaladha yake ya kipekee sana
kaanaga vitunguu mpaka viwe vya kahawia ili kuleta ladha nzuri katika mchuzi wako na kuondoa harufu ya mbuzi ili mtu yeyote yule aweze kula
baada ya kitunguu kuwa kahawia weka nyama ya mbuzi piaendkea kukaanga
ongeza maji kiasi ili sufuria isiungue pamoja na nyama
kisha weka chumvi
acha mbuzi ichemke na itakua na mchuzi wa kahawia
kisha weka kitunguu swaumu hicho ni kifaa maalumu cha kusagia kitunguu swumu
baada yahapo weka viazi uklaya vilivyomenywa safi na kukatwa katwa vidogo
kisha weka nyanya ya kopo
kisha weka mchanganyiko wa mboga majani ( caroti, njegere na pili pili hoho, mahindi machanga ya njano)
kuongeza ladha zaidi unaweza weka unga wa binzali au rojo la binzali
MAFUNZO SAFI KABISA YA CHAPATI NA NYAMA YA MBUZI WAPIKIE FAMILIA YAKO CHAKULA BORA NA SALAMA WAFURAHIE
18 comments:
Mume wangu anavyopenda chapati kwa maharage! ebu tupe recipe za chapati tupate kuongeza ujuzi.
Mbuzi itakuwa kiongezeo poa katika mlo huo.
Asante bro.
kAKA HIZO RECIPE ZIKO WAPI? UNATUJAZA MATE TU MIDOMONI1
Tafadhali nitumie hiyo ratiba ya chakula cha mtoto maana vyakula vyote nanunua lakini mtoto wangu ana upungufu wa damu, pengine lishe siyo well controlled. Ntashukuru sana kwa hilo
kaka twaomba basi hizo recipe asante kwa kazi nzuri uifanyaoyo.
atleast kila picha iwe captioned
Tunaomba maelekezo kaka Chef!!!!
Woow nimependa sana style ya kukata chapati sijawahi ona natumia muda mrefu kufanya madonge madogo then nasukums naweka mafuta bt hiyo yako safi sana nasubiria sambusa maana kuzikunha style nying thanks sheffffff ybty
Asante hiyo style ya kukata chapati nimeipenda ni rahisi sana.
Mimi uwa situmii mafuta kupika roast ya nyama lakini naenda steps kama zako. Asante sana.
Natengeneza nyama yangu, na kutayarisha vitu vingine.
Naichangaya na kitunguu maji, pili pili Manga ya unga, chumvi then nachemsha bila kuweka maji kwanza.
ikishaanza kukauka yale maji yake naongeza maji kwa kiasi ikiiva na kukaribia kukauka, naweka nyanya ya tunda, mbatambata (viazi ulaya) na kitunguu saumu, na nyaya ya paketi, naendelea kuchemsha mpaka nyanya ziive vizuri na kuangalia roast iwe ya kutosha.
Ikibaki kama dakika 5 kutoa ndiyo naweka karoti, hoho, na curry powder.
I hope niko sahihi kaka.
mama yangu ni mgonjwa anakula mafuta mara chache na kidogo sana na sunflower/oliveoil tu.
Ahsante sana kwa upishi wa chapati maana umenipa mbinu mpya ya kusukuma unga wote uliokandwa, kupaka mafuta, kukunja na halafu kukata vipande. Kwa kweli hii inarahisisha kazi badala ya kukata donge moja moja. Ubarikiwe sana.
sijaelewa hapo katika chapati umesema mayai lakini hujatuelekeza yameenda wapi kwani chef hujasema tuyaweke wapi.please chef sie wengine ni copy and peste...
Asante kwa kuweka mazingira mazuri ya kiafya hii ni habari mpya toka kwangu kuhusu blog blog yako iko poa sana lakini jitahidi kuiboresha zaidi ipendeze hata mimi blog ninayo ila bado nahisi haijapendeza nafikiri kama unaushauri naomba unishauri bado sijamwambia Mr michuzi aitangaze lakini nategemea kuiboresha kama unaitaji kuiona tembelea www.mwangajamii.blogspot.com au kunipa ushauri niandikie ujumbe kwa barua pepe noellsaidi@gmail.com ushauri wako utaniweka karibu na wewe daima ubarikiwe kwa kuelimisha na kufundisha mapishi bora.
Asante kaka. nimepata mbinu mpya na rahisi ya kupika chapati!!
THANKS ALOT ISSA YAANI NILIKUA SIJUI KUPIKA CHAPATI NZURI NILIKUA NAONA NI KAZI NDEFU BUT WITH THIS WATANIKOMA UBARIKIWE
i love u bro kweli ubarikiwe blog yako imenifundisha mengi sana
love uuu
gud job aisee.. thumb up.
hey chef, hiyo mbuzi haitakua ngumu km usipoichemsha kwanza?? i love cooking am gladdy i hv found this group
Issa asante sana kwa kutufundisha kupika, mimi familia yangu hupenda sana Chapati. Sasa nimepata njia mpya ya kupika kwa urahisi kidogo badala ya kukunja moja moja kumbe naweza sukuma msukumo wa kwanza kwa mara moja.
nashukuru kwa kipindi chako kwa lishe za watoto naomba unitumie ratiba kwa mtoto wa miezi tisa hadi mwaka mmoja via josepheva95@yahoo.com,ratiba ya mtoto wa miaka miwili nakuendelea via pninje@yahoo.com
Post a Comment