CHICHILI ZA MIHOGO.
MAHITAJI:
Unga wa mhogo Vikombe viwili
Sukari Robo kikombe
Mafuta (Margarine) Robo kikombe
Yai Moja
Amira Kijiko kimoja cha chai.
NJIA ZA KUTAYARISHA :
1. Pika unga wa mhogo kikombe kimoja katika maji yaliyochemka kiasi cha kikombe kimoja
2. Chekecha unga uliobakia pamoja na amira, kisha ongeza sukari na unga wa mhogo uliopikwa.( sukari siyo lazima)
3. Weka mafuta na changanya vizuri
4. .Ongeza Yai.
5. Changanya vyote kisha kanda kidogo mpaka mchanganyiko umekuwa laini
6. Sukuma kwenye ubao ulio nyunyiziwa unga kisha kata vipande virefu na vyembamba, au kandamiza mchanganyiko kwenye chombo maalum chenye matundu mchanganyiko utumbukie kwenye mafuta yaliyochemka.
7. Kaanga kwenye mafuta mpaka chichili zimekuwa na rangi ya kahawia.
8. Kausha na “Tissue” kuondoa mafuta yaliyozidi.
watoto wengi hupenda kuziita tambi za dengu sasa hizi ni za unga wa muhogo kila mkoa wanamajina yao
INALETWA KWENU NA HAJAT ASIA KAPANDE
2 comments:
Allah azidi kukuweka Inshallah
Asante Hajjat
Post a Comment