CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Thursday, May 20, 2010

UNAJUA MAPISHI YA SAMAKI PWEZA????

SAMAKI HUYU NI MTAMU SANA IKIWA UTAPATIA JINSI YA KUMIPIKA NA MAPISHI HAYA HAYA UNAWEZA TUMIA PRAWNS WA AINA ZOTE, LOBSTA, CHAZA NA UDUVI IWE NI KUTENGENEZA MCHUZI SAFI AU KUTENGENEZA SUPU HATUA ZA MAPISHI NA MAHITAJI NI HIZI HIZI


MCHUZI MZITO WA PWEZA

MAHITAJI

70 gram kitunguu swaumu
150 gram kitunguu maji kata kata
150 gram karoti kata vipande vidogo
1 pilipili ya kijani fresh a pili pili mbuzi
1 kijiko kidogo cha chai unga wa korienda au girigilani
200 gram viazi ulaya
10 gram chumvi
150 gram pilipili hoho
160 gram mafuta ya kupikia
70 gram juisi ya limao
500 gram nyanya ya kopo
350 gram Maji
1 kilo ya pweza kata kata vipande vidogo vidogo

JINSI YA KUANDAA

Weka mafuta katika sufuria kisha acha ya pate moto baada ya hapo weka kitunguu maji kaanga kwa dakika 1 kisha weka kitunguu swaumu kaanga tena kwa dakika 1 kisha weka pweza na viazi ulaya kaanga kwa dakika 10 - 15 kwa moto wa wastani.
 kisha weka unga wa korienda, caroti, pili pili hoho, chumvi, pili pili mbuzi, juisi ya limao kaanga kwa muda kisha weka nyanya ya kopo koroga vizuri kisha weka maji acha ichemke kwa dakika 5 mchuzi upungue itakua imeiva.

JINSI YA KUANDAA SUPU YA SAMAKI PWEZA ( OCTOPUS)

1 Samaki pweza mkate na msafishe vizuri
50 gram kitunguu swaumu
100 gram kitunguu maji chop chop
100 gram kariti kata vipande vidogo
1 pilipili ya kijani fresh
1 kijiko kidogo cha chai unga wa korienda au girigilani
5 gram chumvi
5 gram pilipili manga
100 gram mafuta ya kupikia
50 gram juisi ya Limao
150 gram nyanya ya kopo
1.5 lita ya Maji
1 kilo ya pweza

JINSI A KUANDAA

Weka mafuta katika sufuria kisha kaanga kitunguu maji na kitunguu swaumu baada ya hapo weka pweza kaanga kwa dakika 10 kisha weka viungo vyote vilivyobakia kaanga kidogo kisha weka maji chemsha katika moto wa wastani kwa dakika 15 itakua imeiva mpatie mlaji ikiwa ya moto


Huu ni muonekano wa samaki pweza akiwa amekatwa na kusafishwa vizuri



SUPU YA PWEZA YENYE LADHA YA NYANYA NA LIMAO






KWA WALE WASIOTUMIA NYANYA KWA MATATIZO YA GESI NA KIUNGULIA USIWEKE NYANYA YA KOPO NA SUPU YAKO ITAKUA NA MUONEKANO HUU NA LADHA SAFI KABISA



11 comments:

Disminder orig baby said...

Tupe tupe recipe za shurba tupate kongeza ladha majumbani kwetu.

Anonymous said...

chef i hope hii msg utaipata,nataka uliza if wawez nisaidia recipe za salad zilizojaa viburudisho vya kutosha,jana nlienda sehemu nkapewa salad tamu sanaa nkashindwa uliza muandajai nkasema ntakuuliz ww,ila what i noticed aliweka some white salat dresing,zabibu,carot,salad leaves,tuna fish,tango,cuna some cubes ukitafuna ni kama kaukau fulani kama biscuit,na cubes nyeupe ziko kama cheese ila ni common in salad jina limenitoka,na aliweka olives na nkahisi kulikua na mafuta kwa mbali..naomba unisaidie hii recipe kama una salad ya aina hii

Yasinta Ngonyani said...

Asante sana kwa hili kwani kila siku nilikuwa najiuliza nipikeje huyo samaki. je naweza kubadili badala ya pweza na kutumbia kamba?

Unknown said...

For sure Sinta.

Anonymous said...

Asante chef,nimesubiri hii kitu kwa muda mrefu. be blessed

Anonymous said...

Thanks Issa for ur good rich inputs in our daily Health life.

Everytime I make Passion juice inakuwa na kama kauchachu au uchungu fulani I cant get it right. Will try to blend it with sugar kabisa as you suggested.

Please let us know kuhusu juice ya carrot na nilishasikia Apple + ginger + carrot inafanya a good diet juice can you comment on that and how to prepare it.

La pili ni mawazo tu if possible uanzishe darasa la kujifunza kwa mazoezi kama itawezekana and we mothers, sisters and wives are ready to pay the fee for those classes.Hope men also.

Good work and may God bless what you do always.

ruky said...

Asante shef hapo kwenye supu ya pweza ndio penyewe

Anonymous said...

Nimesikia hii supu inaongeza nguvu kule sehemu sehemu.... hivi ni kweli? Sassa nini kipimo ili tusije tukauana? (nafikiri unanielewa)

Christina D. Ngalo said...

Nakushukuru sana Bw.Chief kwa maelekezo ya kumpika huyo samaki. Nitaenda kujaribu kumpika nikifuatisha maelekezo yako.
Tina Ngalo.

Unknown said...

shef uko juu..

Unknown said...

Hongera shef Issa, swali langu nikuhusu uandaaji wa pweza akitoka kuvuliwa , instead yakumpiga piga na rungu kuna any other way mbayo inaweza kufanyika indoor? Ambayo haita hitaji too much muscle. Any is there a need to beat it with clabs after fishing it