PIE YA MCHANGANYIKO WA MATUNDA
Hii ni nanasi ya kopo
Hii ni nanasi ya kopo na aple lililokatwa vipande vidogo vidogo changanya kidogo na mkate uponde ponde changanya na hayo matunda
Hii ni sweet pastry mchanganyiko na vipimo angalia jinsi ya kutengeneza biscuti vipimo na mnchanganyiko ni sawa. sukuma upate wembamba wa kawaida
chukua chombo cha kutengenezea pie yako kisha kata umbo la duara
baada ya hapo weka mchanganyiko ule wa matunda navipande vya mkate, unaweza tumia matunda ya aina yeyote ilimradi upate ladha safi unayoipenda wewe
KIsha sukuma tena upate wembamba wa kawaida na kata kamainavyoonekana katika picha na unaweza tumia kisu kama huna kifaa hicho
Kisha chukua vipande hivyo na weka juu ya pie yako
Endelea kuweka juu ya hiyo pie kwa nafasi
Huu ndio muonekano safi kabisa wa pie inayoonekana kama drafti
Kumbuka pie yetu ia ladha ya tunda apple na nanasi sasa tunaweka syrup ya trawberry ili kuongeza ladhasafi ya matunda mchanganyiko pamoja na rangi nzuri juu ya pie
Usiweke kwenye unga weka kwenye matundu kama inavyoonekana katika picha
KISHA CHOMA KATIKA OVEN KWA DAKIKA 15 TU NA HUU NDIO MUONEKANO WA PIE YAKO SAFI INAUWEZO WA KUKAA KATIKA FRIJI KWA MWEZI MZIMA NA KUMBUKA KUMPATIA MLAJI IKIWA YA BARIDI
1 comment:
Kaka Issa, hii tunaisubiria kwa hamu.
Post a Comment