CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Sunday, September 5, 2010

KITAFUNWA CHA HARAKA UKIWA NYUMBANI

MAHITAJI KWAJILI MANDA
48O gram unga wa ngano
1 kijiko kikubwa cha chakula samli au mafuta ya kula

5 gram chumvi


MAHITAJI KWAJILI YA MCHANGANYIKO WA NDANI YA MANDA

60 gram kitunguu maji 

1 au 2 pili pili mbuzi chop chop
30 gram kitunguu swaumu

60 gram fresh mozzarella, vipande ( au grated mozzarella)

60 gram nyanya chopchop
1 Tangawizi iliyomenywa na kupendwa pondwa 

1-2 matone ya  rice vinegar (au ya kawaida)

1 fungu la majani ya korienda

chumvi kwa mbali kiasi cha kutia ladha tu JINSI YA KUANDAA SPRING ROLL YA MBOGA MAJANI NA CHEESE FATA MAELEKEZO KATIKA PICHA KWA CHINIHuu ni muonekano wa unga wa ngano safi kabisa tayari kwajili ya kukanda mandaChukua unga wa ngano mafuuta ya kula pamoja chumvi ksaha changanya, weka maji kidogo na changanya tena mpaka upate mchanganyiko mgumu kama unavyoona kwenye picha isiwe laini au tepe tepe.


Kisha chukua mchanganyiko na uanze kusukuma kama inayoonyesha picha


Hakikisha unasukuma mpaka inakua bapa ya wastani kama inavyoonekana kwenye picha. Ikiwa nzito inakua laini sana ikiiva na haivi vizuri mpaka ndani ikiwa nyepesi sana itapasuka wakati wa kukunja iwe wastani ili ikiiva iive mpaka ndani na iwe kau kau.


Kisha kata maumbo ya pembe nne yenye ukubwa sawa kama inavyoonekana kwenye picha


Chukua kikaango na kisha weka mafuta yapate moto baada ya hapo weka mchanganyiko wa mboga zote na vinegar usiweke cheese peke yake na uanze kukaanga kwa dakika 3 tuKisha weka cheese na endelea kukoroga ichanganyike vizuri na mboga majani zilizopo kwenye kikaango kwa dakika 1 tu.

 


Kisha weka kwenye ile manda uliyokata mchanganyiko wa mboga majani na cheese kwa mwisho kabisa wa manda kama picha inavyoelekeza.
kisha anza kufunga kwa pembeni, kisha fatia upande mboga majani zilipo na zungusha kama picha inavyooelekeza.

 


Endelea kuzungusha ukiwa umebana vizuri ili manda ikamate vizuri huo mchangayiko wa mboga na kutengeneza umbo zuri na gumu la mduara.


Huu ni muonekano baada ya kuzungusha mapaka mwisho na kupata umbo safi la mduara.

 

Pasha mafuta katika kikaango na kisha anza kuchoma kwenye mafuta yenye moto wa wastani, yakiwa ya moto sana kitafunwa chako kitababuka na hakitaiva.


Ikisha badilika rangi toa katika mafuta na weka pembeni ipoe kiasi kisha mpatie mlaji na tomato sauce, BBQ sauce, Tartare sauce, Mastard sauce, Chachandu au ukwaju.Baada ya kuiva ukiikata kwa ndani huu ndio muonekano wake.
Inapendeza sana muonekano wake na nirahisi sana kutengeneza na ninafuu sana kwa gharama unaweza fanya utundu kwa kutumia recipe hii usiweke mboga manaji ila ukaweka nyama ya kuku, samaki au ng'ombe ikiwa peke yake au hata kuchanganya na mboga majani na ikatoka safi sana na ukafurahia na familia yako kila kitu ni ubunifu tu.

 

4 comments:

Unknown said...

hii ndiyo tuanitaka kaka, tupe maelezo ya hizo manda tafadhali

Anonymous said...

hongera kwa mapishi ya maana,naomba utuwekee namna yakupika egg chop

Disminder orig baby said...

kaka nisaidie, wakati unasukuma huo ni unga wa ngano au wa mchele?

Anonymous said...

Hongera sana kwa jinsi unavyoelekeza mana unaweka na picha halisi inayosaidia msomaji
Mi naomba utuelekeze jinsi ya kuandaa eggchop