CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Tuesday, September 21, 2010

JIFUNZE KUTENGENEZA WALI WA NJUGU NA NJEGERE

WALI  HUU NI MAARUFU SANA KWA WATOTO HUWA WANAUITA WALI MATUNDA HAHAHAHAAAAAAA!!!

MAHITAJI

240 gram mchele wa basmati rice (au mchele wowote mrefu – pia unaweza tumia wali uliobaki)
360 gram njugu mawe zilizochemshwa
1 kijiko kidogo cha chakula mbegu za binzali nyembamba
1 bay leaf
2 au 3 hiriki nzima za kukauka
2 au 3 mbegu ya karafuu 
1/4 kijiko kidogo cha chai unga wa binzali
1 kitunguu maji chop chop
1 carrot kata kat vipande vidogo vidogo
60 gram mahindi ya njano ya kopo
60 gram njegere za kuchemshwa au za kopo
Chumvi weka kulingana na ladha 
1 fungu la giligilani (fresh coriender) kwajili ya kupambia na kuweka harufu nzuri.


Nakusahuri loweka mchele wako kwenye maji kwa dakika 20. Hii itakusaidia unapopika wali wako usishikane na uive haraka kutoka na na aina ya mapishi haya. Ila tumia njia hii ukiwa na muda tu kama huna muda wakusubiri piaka kawaida. Washa jiko kisha weka kikaango au sufuri ili lipate moto kisha weka kijiko kimoja kikubwa cha mafuta. Ongezea mbegu za binzali nyembamba. Kisha weka vitunguu chop chop kaanga kwa dakika 1 kisha weka, karafuu, mbegu za hiriki, bay leaf , binzali ya unga na chumvi endelea kukoroga ili viive viungo vyote.KIsha ongeza carrots na kaanga kwa 40 sekunde. Kisha weka mchele (Kama uliloweka kwenye maji hakiisha unauchuja vizuri uwe mkavu).endelea kukaanga na hakikisha mchele wote unakua mkavu na kuelekea kuiva.
Kihs weka maji 480gram  (kama wali wako utakua haujaiva unaweza kuongeza maji 240 gram inategemea na ubora wa mchele wako). Funga mfuniko na pika kwa dakika 8-10 mpka wali uive na uone maji yamekauka kabisa. Kisha weka njugu mawe na njegere endelea kukoroga uchanganyike safi kabisa.

 

KIsha mwagia majani ya giligilani (corriender) kwa ldha safi na harufu nzuri. Kama unatumia wali ulio bakia, kumbuka karoti kuziweka pamoja na njugu na njegere wakati wa kupika. 

Kupika wali uliobakia kwanza vile viungo vyote vya mwanzo pamoja na kitunguu weka kama kawaida kaanga kisha unaweka karoti, njegere na njugu mawe kaanga mapaka zilainike kisha unaeka wali na kuendelea kukoroga. pika kwa dakika 3-5 au mapak wali wako ukiwa unamoto wa kutosha na umechanganyika vizuri na mboga zote.KIsha kata vipande vya mkate na uvikaushe kwenye oven au kwenye mafuta na pamnba juu ya wali wako. Sasa itakau tayari kwa kula nakuachi kazi ya kuandaa mboga ya kulia iwe nyama au samaki au hata ukitaka kula hivyo hivyo inafaa sana tu  ;)
 
Huu ni muonekano wa wali uliokwisha iva unapendeza katika sahani

 
CHAKULA HIKI NI KIZURI SANA KWA FAMILIA YAKO!! ONEKANA BORA KWA KUA MBUNIFU WA MAPISHI MBALI MABALI KATIKA FAMILIA YAKO.2 comments:

Anonymous said...

Tunashukuru sana kaka Issa kwa kutupatia hizi recipe za nguvu. Kwa kweli hii ya leo wali umekaa vizuri japo nshakula lkn ilipoona picha nimetamani kula tena.
Bis up sana!
Mdau wa Uchina

Anonymous said...

Issa rudi nyumbani kwetu bongo!! kweli mafunzo tunayapata lakini tunahitaji kuonja live kutoka kwako. Please brother fungua shule au kitu fulani hapa nyumbani. Kwa kuwa vitu ulivyo navyo ni vikubwa na wanafaidi wengine tu! Sisi tunajaribu lakini kuna muda havitokeii kabisa kama vyako.

Asante
Dada anayehitaji live chakula.