CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Tuesday, September 21, 2010

TENGENEZA ICE CREAM YA MAEMBE NA LADHA YA NAZI BILA YA KUTUMIA MASHINE


  RECIPE SAFI KABISA NI RAHISI SANA NA UNATENGENEZA KIASI CHA KUTOSHA KISHA UNAHIFADHI KWA MATUMIZI YA MUDA MREFU KWA FAMILIA.

MAHITAJI

2 maembe makubwa yaliyoiva wastani
2 kijiko cha chai juice ya limao
240 gram tui la nazi iwe ya unga au fresh 
240 gram maziwa ya maji 
3 kijiko kikubwa cha chakula maizena (cornstach)
120 sukari
1/4 chumvi kijiko cha chai  
2 kijiko kikubwa cha chakula machicha ya nazi
2 ute wa yai mweupe
120 fresh heavy cream

JINSI YA KUANDAA FATILIA MAFUNZO KATIKA PICHA HAPO CHINI


Menya maembe yako vizuri na kisha katakata vipande vidogo vidogo na weka katika mashine ya kusagia yasage mpaka upate uji mzito kabisa wa maembe.


 Chukua tui la nazi na nusu ya maziwa kisha weka katika kikaango au sufuri ana yapashe moto.

maziwa yaliyobakia weka katika bakuli nyingine na changanya cornstar chsukari pamoja na chumvi.

Kisha chukua mchanganyiko wa maziwa na sukari weka kwenye mchanganyiko wa maziwa na nazi na endelea kupasha katika moto mdogo sana iwe vugu vugu tu isichemke.

koroga moja kwa moja bila kuacha mpaka mchanganyiko wako uwe mzito kabisa.


 
Kisha ongezea yale machicha ya nazni na weka pembeni ipoe.
Kisha chukua uji mzito wa maembe na changanya katika ule mchanganyiko wako wa maziwa na nazi
Koroga uchanganyike vizuri mchanganyiko wote kama inavyoonekana katika picha
Kisha mimina katika bakuli la kioo na iweke kwenye freezer igande 
Tumia mashine ay mchapo chapa ute wa mweupe wa mayai
 
Hakikisha ute unakua laini mpaka unakau kama mapovu
Kisha piga cream kwa kutumia mchapo au mashine

Kisha chukua ule ute wa mayai changanya na cream uliyopiga tayari pole pole mpaka ichanganyike vizuri.
Kisha chukua ule mchanganyiko wa maembe utakua umesha ganda nusu hamishia katika bakuli safi
 
Kisha chukua ule mchanganyiko wa cream mwagia katika mchanganyiko wa maembe na changanya pole pole.Hakikisha unachanganya pole pole usitumie nguvu utaharibu ni pole pole.

Mchanganyiko wako sasa upo safi kabisa kama unavyoonekana katika picha

Kisha chukua mchanganyiko wako na hamishia kwenye lile bakuli ulilotumia mwanzo kugandishia weka kwenye freezer na igandishe kwa masaa 3. Kisha itoe na ikoroge mpaka iwe laini kabisa kisha irudishie tena mpaka igande kabisa.


Kabla ya kuchota hakikisha kijiko cha chakula au kijiko maalumu cha kuchotea unakiweka kwenye maji moto ili ikurahisicshie kutoshika na kutoa umbo zuri.
Unaweza weka kwenye bakuli na ukala ukafurahia au unaweza weka kwenye biscuit

 Pia unaweza weka kipande cha embe kwa juu kama urembo na ikapendeza kabisa 


HUU NDIO MUONEKANO WA ICE CREAM YETU UNAWEZA WEKA LADHA YEYOTE ILE IWE VANILLA AU CHOCOLATE AU KARANGA NI WEWE BINAFSI UPENDAVYO SIO LAZIMA IWE YA NZAI NA BADO ITAPENDEZA SNA HATA UNAWEZA WEKA LADHA YA MACHUNGWA AU PAPAI AU NANASI FURAHIA HII NA FAMILIA YAKO 

1 comment:

Anonymous said...

Ndugu yangu tunapenda recipe zakon ila hapo kwenye ice creaam ya maembe vitu vingine hatujui ninini manake umeweka picha tu hukuweka maelekezo manake vitu vingine vinafanana na unga wa uji(mahindi)
Thanks
Mdau