RECIPE SAFI SANA YA DENGU HIZI ZA AINA YAKE
MAHITAJI
240gram Pigeon Peas ( Dengu)
1/4 tsp Turmeric (manjano)
720 gram maji masafi
3 kijiko kikubwa cha chakula samli (Ghee)
1 kitunguu kikubwa chop chop
1 nyanya ya kuiva kubwa chop chop
1 kijikon kimoja cha chai binzali nyembamba
2 pili pli kavu nyekundu (Dried Red Chilies)
3 mbegu za karafuu
1 tangawizi ya kusaga (grated Ginger)
majani ya Curry na giligilani kwajili ya kupambia
5 gram maji ya limao
5 gram ya chumvi
JINSI YA KUANDAA CHAKULA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI
Muda wa kuandaa : Dakika 15
Muda wa kupika : Dakika 15
Idadi ya walaji : Watu 4
MAHITAJI
240gram Pigeon Peas ( Dengu)
1/4 tsp Turmeric (manjano)
720 gram maji masafi
3 kijiko kikubwa cha chakula samli (Ghee)
1 kitunguu kikubwa chop chop
1 nyanya ya kuiva kubwa chop chop
1 kijikon kimoja cha chai binzali nyembamba
2 pili pli kavu nyekundu (Dried Red Chilies)
3 mbegu za karafuu
1 tangawizi ya kusaga (grated Ginger)
majani ya Curry na giligilani kwajili ya kupambia
5 gram maji ya limao
5 gram ya chumvi
JINSI YA KUANDAA CHAKULA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI
Muda wa kuandaa : Dakika 15
Muda wa kupika : Dakika 15
Idadi ya walaji : Watu 4
Osha dengu katika maji baridi kisha zichuje vizuri.
Unaweza tumia njia mbili ya kuzipika hizi dengu moja ni kuloweka kwa masaa 2 kisha unazichemsha kwa sufuria ya kawaida au unaweza tumia pressure cooker na ukaweka manjano na kutumia maji gram 720.
Kwa kutumia preasure cooker ni dakika 10 tu zinakua zimeshaiva.
Wakati unachemsha dengu weka kikaango au sufuria ipate moto weka mafuta kisha ongeza samli (Ghee), binzali nyembamba, karafuu, pilipili, tangawizi, kitunguu maji pamoja na chumvi endelea kukaanga.
Vitunguu vinapoanza kuiva ongeza nyanya endelea kukaanga zikiiva weka majani ya curry na majani ya giligilani.
Toa dengu zako katika pressure cooker. dengu zako zitakua zimeiva kabisa na kua na ubora safi kabisa.
Maji yatakua yamekauka katika preasure cooker chemsha maji kikombe kimoja na weka katika preasure cooker na ukoroge.
Kisha chukua ule mchanganyiko wako wa vitunguu na nyanya kisha mimina kwenye dengu zako.
Hakikisha unaendelea kukoroga na ongeza maji ya limao pia kwa kuongezea ladha zaidi.
Hakikisha unampatia mlaji chakula hiki safi kabisa kikiwa chamoto unaweza kula na chapati, mkate, Tortillas, Naan or ugali pia hata wali na familia ikafurahia sana.
Binafsi huwa napenda kula ikiwa pamoja na chapati na wali ili kuongeza ladha na ubora huwa naongeza limao kwakua linasaidia kupunguza madini ya chuma katika dengu.
ANDAA CHAKULA HIKI KIZURI UKIWAPUMZISHA NYUMBANI KULA NYAMA MARA KWA MARA NA WATAFURAHIA KUANZA MWAKA NA CHAKULA SAAFI
2 comments:
inavutia lakini mbona hautuwekei maelezo jinsi ya kupika na mahitaji? please tunakuomba uweke......
Mdau wako
Arusha
inapendeza ukiiona ila naomba uwe unatuwekea maelezo jinsi ya kupika kutuonyesha picha haitoshi.
mdau wako Dar
Post a Comment