CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Saturday, March 30, 2013

JIFUNZE JINSI YA KUPIKA MKATE HUU MWEUPE

JIFUNZE KUTENGENEZA MKATE HUU MWEUPE NI RAHISI NA NAFUU KUANDAA ONYESHA UJUZI WAKO KATIKA FAMILIA
 
MAHITAJI
 
1 kg unga wa ngano
2 kijiko kidogo cha chai chumvi
240 gram maziwa ya maji ya vugu vungu
60 gram maji ya vugu vugu
2 kijiko kikubwa cha chakula siagi, iyeyushe
3 kijiko kikubwa cha chakula asali
2 kijiko kidogo cha chai amira ya chenga

JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI
 
Muda wa maandalizi : Masaa 2 hadi 4
Muda wa mapishi : Dakika 30 hadi saa 1
Idadi ya walaji : Watu 4
Ujazo : Unapata mkate wenye 9-inch
 
 
Chukua robo tatu ya unga pamoja na chumvi kisha chukua mchapo na uchanganye. 

 
 Chukua bakuli safi kavu kisha changanya maziwa, majina, siagi, chumvi pamoja na amira. Hakikisha joto la maziwa na maji liwe 110 degrees.

 
 Mimina mchanganiko wako wenye maziwa katika unga.

 
Anza kukanda pole pole 

 
Hapa mchanganyiko wako umeshaanza kushikana. 

 
Chukua mchanganyiko wako kisha weka juu ya meza hakikisha umemwagia unga kwa juu endelea kukanda vizuri kwa dakika 10.

 
Kama unafikiri mchanganyiko bado una maji maji, basi chukua robo ya unga iliobakia tumia kijiko kikubwa cha chakula ongeza kimoja kimoja epuka kuweka unga wote ukazidisha.

 
Chukua bakuli safi na kavu, kisha lipake mafuta na weka mchanganyiko wako katika hiyo bakuli. 

 
KIsha tumia plastic na funika weka sehemu yenye joto, jikoni kuna joto.

 
Hakikisha mchanganyiko wako umeongezeka mara 2, ndani ya dakika 40 mpaka 50. 

 
Kisha chukua mchanganyiko wako ukande vizuri na weka katika chombo chako cha kuokea kiwe cha chuma au cha kioo kama changu chenye ukubwa wa  8.5 X 4.5 X 2.5 (1.5 Lita).

 
 Kisha funika tena kwa plastic

 
 Weka pembeni kwa dakika 20 mpaka 30 itakua imeshaumuka vizuri kama unavyoona katika picha weka katika oven.

 
 Kumbuka oven yako unatakiwa uiwashe kabla katika joto la 350 degrees, ukishaweka unga katika oven unaweza rushia maji kidogo ili kuweka mvuke utakao saidia kuweka rangi nzuri ya brown na kua na gamba gumu. Oka kwa dakika 40 mpaka 50 mkate wako utakua umeiva.

 
Toa mkate wako katika pan, hamishia katika wire rack, ili mkate uweze kupoa.

 
Kata kata vipande na wapatie walaji, unaona mkate ulivyochambuka. 

 
Unaweza ukavuta picha huu mkate ni mtamu kiasi gani ukishapaka siagi kwajuu? au ukipaka jam pia? Ni mtamu sana sana.
 


4 comments:

Anonymous said...

ASANTE SANA KWA MAPISHI YA MKATE HUU. GOD BLESS.

Anonymous said...

CHEF TUNAOMBA MAELEKEZO KWA MAANDISHI HIVI VYA PICHA TU HAVITOSHI, TAFADHALI. UBARIKIWE SANA

ELINE

Anonymous said...

Habar chef nataka kujifunza cakes, niwe proffesional kwny hili kanin cjui på kupata elimu. Naomba nisaidie chef. Ubarikiwe xana

mama abdulrahman said...

Ahsante sana kwa mapishi hasa ya mkate huu,nimefuatilia hatua zote na vipimo, nashukuru sana umetoka vizuri, nimeandaa kwa futari ya leo,shukran. mwenyeezi mungu akuzidishie ujuzi.