APPLES Protects your heart, prevents constipation, Blocks diarrhea, Improves lung capacity Cushions joints
APRICOTS Combats cancer, Controls blood pressure ,Saves your eyesight ,Shields against Alzheimer's ,Slows aging process
ARTICHOKES Aids digestion, Lowers cholesterol, Protects your heart, Stabilizes blood sugar Guards against liver disease
AVOCADOS Battles diabetes, Lowers cholesterol, Helps stops strokes, Controls blood pressure Smoothes skin
BANANA Protects your heart, Quiets a cough, Strengthens bones, Controls blood pressure, Blocks diarrhea
BEANS Prevents constipation, Helps hemorrhoids, Lowers cholesterol, Combats cancer, Stabilizes blood sugar
BEETS Controls blood pressure, Combats cancer, Strengthens bones, Protects your heart, Aids weight loss
BLUEBERRIES Combats cancer, Protects your heart, Stabilizes blood sugar, Boosts memory , Prevents constipation
BROCCOLI Strengthens bones, Saves eyesight, Combats cancer, Protects your heart, Controls blood pressure
CABBAGE Combats cancer, Prevents constipation, Promotes weight loss, Protects your heart, Helps hemorrhoids
CANTALOUPE Saves eyesight, Controls blood pressure, Lowers cholesterol, Combats cancer Supports immune system
CARROTS Saves eyesight, Protects your heart, Prevents constipation, Combats cancer, Promotes weight loss
Unaweza badilisha tabia ya mtoto wako au mtu yeyote unaeishi nae nyumba moja asiyependa kula mboga majani au matunda kwa kubadilisha muonekano wa chakula hicho au tunda hilo kwa kulinakshi kwa mtindo wowote ule ilimradi kionekane kitu tofauti na kinachovutia hii itakua njia rahisi sana kumvutia mtoto au mkubwa chakula kizuri au upambaji wa chakula sio mpaka hotelini hata nyumbani unaweza fanya sanaa hii na wala haiitaji muda mrefu wa maandalizi muonekano bora wa chakula hutia hamasa kwa mlaji leo tutaangalia utengenezaji wa salad na kuipamba na uandaaji wa mboga ktk muonekano wa kuvutia upande wa kuchonga matunda tutaangalia wakati ujao fata maelezo jinsi ya kutengeneza salad yenye mchanganyiko wa mboga mboga hapo chini.
Hili ni jokofu la kutunzia mchanganyiko wa mboga katika nyuzi joto 4 hadi 5 tu kwa hali ya usalama sana kwa manufaa na afya ya mlaji tukianzia juu kushoto ni mahindi mabichi ya njano kabla huifadhiwa katika kopo tayari kwa matumizi, karoti iliyokwaruzwa, Lime stone lettuce, chicory, Radish iliyokwaruzwa, zucchin iliyokwaruzwa, rollo nyekundu, rollo ya kijani, matango yaliyokatwa, celeriac salad, curly endive, chicory nyekundu.
Katika sahani yako anza kupanga mboga ambazo zimekatwakatwa ambazo ni karoti, matango, mahindi machanga ya njano, celeriac salad na radish nyeupe
Chota kidogo kidogo kila moja panga kwa mtindo wa duara nusu sahani tu kama mduara wa nusu mwezi kati kati acha nafasi kiasi.
Baada ya hapo chukua jani la salad moja moja toka kila aina ya salad pagange sambamba majani hayo kisha zungusha yabane kama unataka kuyafunga kamba kisha kata kiasi upande wa chini utakua umepata kitako safi utakua umetengeneza kama uwa rozi.
Kisha liweke juu ya zile mboga mboga pembei yake kata kipande cha tikiti maji rangi yeyote ile kama ni la kijani, jekundu au rangi ya chungwa pamba kama invyoonekana katika picha.
Kisha kata slice nyembamba ya chungwa katikati yake weka tunda lolote dogo la mviringo kama zabibu au strawbery chomeka toothpick ili ishikilie chungwa juu ya tikiti maji.
Salad hii unaweza mwagia dresing yeyote ile mfano italian dressing, french dressing au siki na chumvi inatosha salad hii unaweza kula na kipande cha kuku, samaki wakuchemsha au wa kukaanga na unakua umekula mlo safi kabisa bila stach kwa watu wanaofanya dayati hapa ni mahala pake mvuto na muonekano wa sahani utamfanya mlaji avutie hata kama si mpenzi wa mboga na matunda.
Hili ni jokofu la kutunzia mchanganyiko wa mboga katika nyuzi joto 4 hadi 5 tu kwa hali ya usafi sana kwa manufaa na afya ya mlaji tukianzia juu kushoto ni nanasi iliyopikwa katika sukari, embe mafuta, cappers, vitunguu vidogo vya kopo, chopped chives, chopped onion, olives nyeusi, asparagus, matango machanga yaliyosindikwa, olives zakijani, Nyanya
Katika sahani yako anza kupanga mboga ambazo zimekatwakatwa ambazo ni karoti, matango, mahindi machanga ya njano, celeriac salad na radish nyeupe.
Chota kidogo kidogo kila moja panga kwa mtindo wa duara kuzunguka sahani yote katikati acha nafasi.
Baada ya hapo chukua jani la salad moja moja toka kila aina ya salad pagange sambamba majani hayo kisha zungusha yabane kama unataka kuyafunga kamba kisha kata kiasi upande wa chi utakua umepata kitako safi utakua umetengeneza kama uwa rozi.
Kisha liweke pembeni ya zile mboga mboga katikati ya sahani unaweza weka mchanganyiko wowote ule wa nyama ya kuku, ngo'mbe, samaki au sausage iliyochemshwa ikapoa.
Kata saizi ya kuweza kuingia mdomoni kisha changanya na vitunguu vilivyochopiwa safi pamoja chives.
Mchanganyiko huo unaweza malizia na chaguo lako la dresing yeyote uipendayo kisha unamwagia kati kati ya sahani mwisho kata nyanya kipande weka pamoja na tango dogo la kopo na olive moja ya kijani na moja nyeusi kwa kupamba salad yako.
Kwa upande wa mlo kamili baada ya kupika chakula chako kikaiva kama ni ugali au wali
Chemsha njegere zisiive sana
Kisha kata vitunguu vidogo sana kaanga katika siagi dakika 1 tu
Kisha weka hizo njegere zilizoiva katika sufuria kwa dk 2 usiasahau chumvi kisha zitoe
Chukua nyanya nzuri ngumu iliyokwisha iva kata nusu pia kata kidogo katika kitako ili iweze kukaa katika sahaki
Kisha toa mbegu zote katikati ya nyanya tumia kijiko kuchota na jaza zile njegere kwanye nyanya
Kisha save nyanya hiyo yenye njegere kama mboga majani itakayo ambatana na chakula chako kama ni cha mchana au cha usiku.
Muonekano na mchanganyiko wa rangi inakua kivutio kizuri sana kwa mtu asiependa kula mboga majani.
Sasa hapa ndio utawakamata kweli kweli wasiopenda kula mboga za majani,
Chukua maharage mabichi yachemshe kiasi yasiive sana yabaki na rangi yake nzuri ya kijani
Kisha unachukua bacon slice zipo aina mbili zipo bacon za nguruwe na bacon za ng'ombe chaguo ni lako mlaji.
Kisha chukua maharage hesabu kumi na tano kisha zungushia bacon katika maharage hayo weka katika ubao wa kukatia kata ncha za mwisho ili kuweka usawa na muonekano mzuri zaidi.
Ukishamaliza weka kikaango kwenye jiko la moto wa wastani tu weka mafuta kiasi katika kikaango yakishapata moto weka maharage yaliyozungushiwa bacon kaanga kiasi tu ili ile bacona ikauke.
Kisha toa tayari kwa chakula pia sevu kama mboga majani itakayo ambatana na chakula chako kama ni cha mchana au cha usiku. Muonekano na mchanganyiko wa rangi inakua kivutio kizuri sana kwa mtu asiependa kula mboga majani.
KWA KUFATILIA MAELEZO HAYA YOTE UTAKUA UMEFANIKIWA KUMREKEBISHA KAMA NI MUME AU MTOTO ASIEPENDA KULA MBOGA ZA MAJANI AU MATUNDA IKIWA UMESHAFAHAMU PIA UMUHIMU WA VYAKULA HIVYO KWA BINADAMU
Nashukuru sana mdau aliezungumzia upatikanaji wa bacon ya ng'ombe, nikweli kwa ulaya kupata bacon ya ng'ombe ni adimu sana ila hapa kwetu Tanzania zinapatikana kwa wingi ukienda katika supermaket kubwa au maduka makubwa ya nyama utapata.
Endapo umekosa basi chukua mboga hiyo hapo juu inaitwa leeks kata jani lake lisafishe vizuri kisha zungushia vizuri maharage yako hatua za upishi ni zile zile unaikaanga kidogo tu itaiva na italeta harufu nzuri sana kwahiyo kwa asie kula kabisa nyama atakua nae kafaidika.
10 comments:
hongera sana chef issa kweli utasaidia wengi n\sasa jikoni kielweka husband atabloo
Kaka mi nakushauri tena tafadhali usizitoe recipe mapema nasisi tuanokwenda internet cafe mara 1 kwa wiki tuweze kusoma zingatia sana hili
Kaka mi nakushauri tena tafadhali usizitoe recipe mapema nasisi tuanokwenda internet cafe mara 1 kwa wiki tuweze kusoma zingatia sana hili
I understand weye ni chef yeah,ila kwa ushauri wangu hayo mambo ya bacon kwakweli hilo ni jambo la kuzingatia sana kwani km nchi hizi za ulaya sidhani km waweza pata bacon ya ng'ombe,okey ndio bacon yaweza kuwa ng'ombe ama nguruwe ila haswa haswa mimi ninacho fahamu huwa ni ya nguruwe,kwani ata maduka ya Halal hawauzi hizo mbona so hebu angalia hilo swala uzuri brav..
Mdau uliezungumzia swala la bacon ni kweli kabisa kwa ulaya ni ngumu sana kupata bacon ya ngombe ila kwa africa unapata bacon ya ngombe inauzwa superamaket kibao au maduka makubwa ya nyama kwa ndugu zangu wa ulaya inakuangumu kidogo kama huli nguruwe lakini nitawapa njia nyingine yakufanya uweze kufaidi pishi hilo hilo bila ya kutumia bacon askhsante sana mdau Chef Issa
Mimi nasubiri recipes za starter nyingine kama soups, na vyakula vidogo vidogo vya kushika mkononi wakati unasubiria mlo, hasa ukiwa una ka dinner party kako, sijui wenyewe wataalamu mnaitaje. Ila kwa kweli pamoja na upenzi wangu wa mapishi hayo mapishi ya mboga mboga ni babu kubwa nashukuru kwa hilo darasa, na Mwenyezi mungu atakulipa ujira mkubwa maana utaokoa ndoa za wengi. Wanaume ugonjwa wao mkubwa chakula, kama kinapikwa na kuandaliwa tofauti tofauti kila siku, basi weekend hatoki, na siku za kazi atarudi mapemaa!! Baada ya ulimi kuridhika na tumbo kushiba akishapata utulivu atatoka aende wapi. Shukran bwana Issa kwa darsa na nusra!
wadau wa ulaya mie ni mkristo pure ila huyombuzi katoliki simtafuni hata kwa dolari huwa natumia bacon za turkey ni nzuri sana nafikiri kwenye hizo mboga labda uweke bacon za turkey na imani itakuwa poa tuu mdau canada
Nakuomba utoe mapishi ambazo chakula ama aina ya mboga inapatika huku kwetu tanzania...kuna vyakula zingine Tanzania hakuna kabisa.. sasa jitahid sana utupe vitu zilizoko huku kwetu.. Pia hakuna maneno ya Kiswahili ya mboga hizi unazoonesha?
kaka am so happy with your blog because i hv taste for food ila sijui kupika kivilee my bro is a chef arusha ila kilasiku yuko porini sasa wewe umekuwa mkombozi wangu wakupika.
Thanx bro
kaka issa wewe ni chef wa kiislam nguruwe umeharamishiwa end of story.
Post a Comment