CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Saturday, July 10, 2010

MAPISHI MBALI MBALI YA SAMAKI AINA YA TROUT

CHAKULA HIKI NI KIZURI SANA KWA AFYA YAKO WEWE MLAJI KAA TAYARI KWA RECIPE

MAHITAJI

1 fungu la majani ya cerely
2 vikubwa kitunguu maji
3 kubwa karoti
4 samaki anina ya trout
1 fungu majani aina ya dill
50 gram kitungu swaumu
2 limao kubwa kamua maji yake
1 chupa ndogo ya fish masala
250 gram mafuta ya kupikia
5 gram pili pili manga
10 gram chumvi


Haya  ni majani ya cerely yanapatikana popote sokoni au duka la mboga kwa urahisi sana na ninafuu husaidia kukata shombo ya samaki na huleta harufu safi sana


Huu ni muonekano wa mkato unaotakiwa kwajili ya caroti za kupikia samaki wako




Huyu ndie samaki hasa nayeitwa trout hupatikana toka maji baridi kwa nyumbani tanzania utampata Arusha ni mzuri na mtamu sana ingawa anamibamidogo midogo sana

JINSI YA KUANDAA

Chukua samaki wako hakikisha ni msafi umetoa magamba na matumbo yote na umemuosha vizuri kwa maji baridi.

Kisha weka karoti kitunguu na cerely kwenye chombocha kuokea na baada ya hapo muweke samaki juu ya hizo mboga mboga kwenye chombo utakachotumia kuokea changanya mafuta ya kupikia, maji ya limao, fish masala, kitunguu swaumu, pili pili manga pamoja na chumvi.

Kisha mwagia juu ya samaki na mwisho kabisa weka majani aina ya dill juu ya samaki funika kwa juu kwa kutumia aluminium foil oka kwenye oven kwa dakika 20 kisha toa hiyo foil acha wazi choma kwa dakika 10 hadi 15 kisha mtoe samaki atakua tayari kwa kuliwa .


Huu ni muonekano wa samaki wakiwa tayari ameshaiva toka kwenye oven na tayari kuliwa


Jinsi ya kupanga katika sahani chota ule mchuzi weka kwenye sahani iliyo kama bakuli kisha chota samaki muweke ndani ya sahani yako, kisha chota majai ya cererly na karoti zilizoiva pamoja na samaki weka juu ya samaki mwisho pamba na jani fresh aina ya dill. Furahia chakula hiki pamoja na famila yako.

AINA HII YA UPIKAJI UNAWEZA TUMIA KWA KUKU AU SAMAKI AINA YA KIBUA, CHANGU, JODARI, SARADINI, RED SNAPER, SATO AU SANGARA.


3 comments:

Anonymous said...

Kaka ss watu wa TBR tunamwita KUKURU

ruky said...

Asante kwa pishi la samaki

Anonymous said...

Habari kaka ansate kwa kazi nzuri kupitia kwako naiboreha ndoa yangu.sasa kaka mimi nipo huku udhunguni ila kuanzia sept natakiwa nihamie bongo na shemejio. sas huku niliko shemijio hupenda sana kutumia soure bread, sijui nimepati sour bread, je naweza nukiwa kwetu aendelee kuenjoy je unaweza nipa recept zake jinsi ya kuundaa mkate huu. nitashukuru kaka, asante sana.