CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Friday, May 28, 2010

MAANDAZI YA HILIKI NA TUI LA NAZI

MAANDAZI HAYA YANALADHA SAFI SANA KWA MLAJI NI RUKSA KUONGEZA KIUNGO AU KUPUNGUZA NA ANDAZI LAKO LITABAKI NA UBORA ULE ULE MAANA SIO WATU WOTE WANAPENDA VIUNGO.
MAHITAJI

1 kikombe cha chai kikubwa
2 Amira ya chenga kijiko kidogo cha chai
1 kilo unga wa ngano
1 hiriki kijiko kikubwa cha chakula
1 kikombe cha chai tui zito la nazi na vijiko viwili vya mafuta ya kupikia ya baridi (1 kikombe cha chai mafuta ya moto kamahutumii tui la nazi )
1 chumvi kijiko kidogo cha chai
1 maji ya moto wa wastani kikombe kikubwa cha chai


Hii ni hiriki , sukari na Amira ya chenga

Weka sukari, Amira, chumvi na hiriki katika bakuli kisha weka mafuta yakupikia vijiko viwili

kisha weka tui la nazi

Kisha changanya unga wa ngano kilo moja katika bakuli

kisha weka maji ya moto katika unga

Anza kukanda unga

Kisha sukuma unga mpaka upate unene wa saizi ya andazi unalotaka 

Kisha kata andazi kwa saizi ya andazi la ukubwa unaotaka

Haya ndio maandazi mabichi baada ya kukatwa tayari kwa kuchomwa acha yaumuke kwa dakika 10 ili utakapochoma yasijae mafuta ndani

Weka mafuta ya kupikia katika kikaango kisha yapate moto wa wastani yasiwe yamoto sana maandazi yakaungua pia hayataiva ndani


HUU NDIO MUONEKANO SAFI WA MAANDAZI YA HIRIKI NA TUI LA NAZI ENJOY NA FAMILIA YAKO KWA CHAI YA JIONI AU CHAI YA ASUBUHI KWA KITAFUNWA SAFI NA SALAMA MAANA HAKINA MAFUTA MENGI PIA CHUMVI INAAIDIA KUKIMBIZA MAFUTA KATIKA UNGA.



10 comments:

shamim said...

hehee nasubiria kwa hamu sana.asante kwa mapishi chef

Anonymous said...

asante sana kwa mapishi murua, yummy yummy.

Naomba kusahihisha kidogo maadhishi au matamshi ya maneno. Sahihi ni hiliki na hamira sio hiriki wala amira.

Unknown said...

Zeze mandazi unashushia roast ya Mbuzi kwa maharage. Na juice hapo loh.

Anonymous said...

sasa mbona katika mahitaji hukutaja sukari?lakini kwenye mchakato wa kutengeza maandazi ipo??

Anonymous said...

Upo juu mwanangu. Mimi mwanaume tena huwa sifatilii mambo ya mapishi lakini hii blog yako inanifanya nibadilike. Kwa mtindo huu lazima niongeze viwango vya mapishi

Anonymous said...

Habari, mbona Mimi nimefata michakato wako maandazi yangu yanatoka Kama yana vipere, sijui wapi nakosea

Anonymous said...

Hi Kapande,

I editted wikipedia and added your link in IT, ial watanzania tuanze kuwa active na kuedit vitu kama wikipedia maana nilikuta wakenya wamejiweka kwamba origin ya Maandazi ni Kenya tu which was not right.

Anonymous said...

Hakikisha unakanda unga hadi unakuwa mlaini na hauna Gisele wala. Madonge

Unknown said...

Aisee Issa. Pongezi sana.Kwa kuwa unaishi Majuu kama mpishi na mtu wa afya ningekuomba pia ukiweza, jaribu kuwafungua macho wenzetu nyumbani kuhusu suala la athari za Gluten katika ngano. Hili tatizo limewabughudhi Wazungu kiasi ambacho sasa hivi tatizo la tumbo (Irritable Bowel Syndrome- yaani IBS) limeenea kila jamii. Husababisha mbali na saratani ya tumbo, mashuzi ya kila mara. Ushuzi ni jambo asilia, lakini kuwa na ushuzi unaonuka sana kila wakati si sawa. Gluten imesemekana kama adui wa chakula miaka ya karibuni. Nimelitaja maana hapa tunazungumzia chapati na maandazi tunayoyapenda. Unga wa ngano ubna Gluten, yaani kile kitu kinachoufanya uvutike. Ni mzuri hasa ukiwa wa rangi kikahawia kuliko ule uliokobolewa mweupe. Pia kupunguza sukari kwa wingi na kutorudia kutumia mafuta ya kupikia mara nyingi nyingi. Hebu tafiti zaidi ndugu yangu Issa. Najua unajali taaluma yako na tuko nyuma yako. Tuna fahari kwa kazi yako. Mafanikio yako ni yetu sote. Na si wapishi wengi wa Kitanzania wanaoipenda au kuithamini kazi yao hivi!

Anonymous said...

Asante sana Kaka Issa kwa mapishi ya maandazi. Nilikuwa sijawahi kupika maandazi katika maisha yangu lakini baada ya kufuata maelekezo yako nlitoa kitu kisicho cha kawaida, na kila aliyekula alisifia sana. Asante sana Bro kwa kuniongezea maujuzi.