CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Wednesday, August 25, 2010

JIFUNZE KUTENGENEZA FRUIT TRIFLE

SAFI SANA KWA FAMILIA YAKO, INALIWA BAADA YA MLO KAMILI NI NZURI SANA NA RAHISI KUTENGENEZA

MAHITAJI

500 gram Mchanganyiko wa matunda angalau anina nne au tatu
500 gram fresh cream
1 box na Biscuit za aina tofauti aidha nyembemba ndefu au za mduara
1 bakuli la kioo linapendeza zaidi
300 gram Keki
200 gram Caster sugar


JINSI YA KUANDAA

Piga kwa kutumia mchapo au mashine fresh cream yako na sukari  mpaka iwe nzito kabisa kam povu  kisha iweke kweny friji ipoe zaidi na kua rahisi kuitumia

Kata matunda yako yeyote yale uliyonayo nusu ili kua na muonekano safi unapo yapamba kwenye bakuli lako.
  


Trifle hii ni ya mchanganyiko wa matunda menya na katakata vipande vidogo vya nanasi, water melon, chungwa na papai unaweza ongezea na apple.

Chini kabisa ya bakuli weka vipande vya keki aina yeyote ile kutokana na ladha unayopenda wewe kisha juu yake panga matunda ukimaliza mwagia kwa juu ile fresh cream uliyokwisha ipiga  sambaza vizuri isibaki nafasi ifunike kabisa matunda yako.

Baada ya hapo weka tena matunda na mwisho mwagia tena fresh cream na usambaze kama mwanzo juu kabisa pamba vizuri kwa biscuit na matunda kama picha inavyoonyesha.

Hapa inakua tayari kwa kuliwa iweke kwenye friji ipate ubaridi safi kisha wapatie walaji wafaidi.PEACH AND RASPBERRY TRIFLE

MAHITAJI

1 Peach ya kopo
200 gram Raspberry
200 gram keki
200 gram Fresh cream
100 gram Sukari

JINSI YA KUANDAA

Kama mwanzo piga fresh cream na sukari kisha anga vipande vya keki na kisha weka matunda aina ya peach  na juu yake weka cream. Rudia tena zoezi hilo na mwisho weka mduara wa peach na kati kati weka raspberry na ju u yake weka fresh cream weka kwenye friji ipoe na wapatie familia wafurahie.
 STRAWBERY TRIFLE
( hii safi sana kwa wano ogopa kupata vitambi au kuongezeka uzito lakini wanapenda kula vizuri)

MAHITAJI

5 gram Cinamon
1 Chungwa lililoiva safi
20 gram sukari
5 gram Vanilla essence
 50 gram keki
5 pc Strawberry fresh
100 gram Fat free cream

JINSI YA KUANDAA

Changanya vanilla, juisi ya chungwa, fat free cream, sukari na cinamon ya unga kwenye blenda mpaka upate mchanganyiko safi mzito.

Kisha kata kata vipande vidogo vya keki kwenye glasi yako ya kioo weka nusu ya glasi na kisha panga strawbery kwa juu.

mwisho mwagia ule mchangayiko wako uliosaga kwenye blenda mimina pole pole mpaka ufike chini ya glasi kama inavyoonekana kwenye picha.

Weka katika friji ipoe, wakati wa chakula mpatie kila momoja glasi yake peke yake afurahie. MIXED BERRIES TRIFLE

MAHITAJI

200 gram Raspberryies
200 gram Starwberries
200 gram Blue berries
2 box finger biscuits
1 jani la mint
100 gram sukari nyeupe safi
1 lita ya fresh cream


JINSI YA KUANDAA

Kama kawaida piga fresh cream na sukari na kisha weka katika friji ipoe

Chini kabisa ya bakuli lako panga finger biscuit kumbuka kuzikata nusu usiziweke zikiwa ndefu kabisa.

Kisha mwagia cream juu yake na sambaza vizuri kabisa.

Kisha panga strawberru ulizozikata nusu kama inayoonekana katika picha  hapo chini.

Kisha mwagia kwa juu fresh cream.

Juu yake panga blue berries safi kabisa.

Juu yake mwagia fresh creama na sambaza vizuri kabisa kisha juu yake panga biscuit na raspberries pamoja na cream kidogo kati kati kabisa mwisho pamba na jani la mint.SIO KAZI NGUMU KABISA UKIFATILIA MAFUNZO VIZURI PAMOJA NA PICHA PIA MAHITAJI YOTE HAYA YANAPATIKAMA KATIKA SUPERMARKET AU MADUKA YA VYAKULA NA MBOGA MBOGA SIO GHALI JITAHIDI SIKU MOJA MOJA WAFURAHISHE FAMILIA YAKO.2 comments:

Disminder orig baby said...

huku kwenye kitindamlo uwe kuna raha yake, asante kaka

Anonymous said...

m mungu akupe afya njema uendelee kutupa mambo mazuri.

naombi naomba unisaidie kuna desert nimeila ipo kama vile castard lakini ni soft saana nafkiri ni aina mbili flan za cream alafu juuu imemwagiwa na kitu kama kokoa ama ni kahawa flani hivi nzuuuri . je kitu hii ni desert gani najua una idea na vitu vingi .pls jinsi ya kuiandaa

ilove curinarychamber