CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Monday, August 23, 2010

SALAD NZURI KWA AFYA YAKO WEWE MLAJI

MAHITAJI

1 paketi ya Spagheti
2 Nyanya
1 kitunguu
1 lettuce
150 gram Balsamic vinegar
5 gram Chumvi
5 gram Pili pili manga
1 Tango


JINSI YA KUANDAA

Chemsha spagheti isiive sana iive kiasi tu ili iwe ngumu na ipendeze katika sahani na kuleta ladha safi kwa mlaji

Ikisha iva weka pembeni ipoe na baada ya hapo changanya chumvi, pili pili manga na balsamic vinegar pamoja na hiyo spagheti.

kisha kata slice ya nyanya, tango pamoja na kitunguu kama inavyoonekana kwenye picha.

weka jani la lettuce kwa mbele kisha kati kati ya sahani weka mlima mdogo wa spagheti iliyokwisha changanywa, kwa nyuma weka slice za tango na kwa juu weka slice ya nyanya na kitunguu.Huu ni muonekano wa salad yako kwa juu ikiwa imekamilika tayari kwa kumpatia mlaji


Muonekano huu kwa pembeni salad safi ya tambi na mboga majani waandalie familia wafurahie.


No comments: