CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Sunday, August 1, 2010

JINSI YA KUTENGENEZA BLACK FOREST CAKE

KAA TAYARI KWA RECIPE SAFI KABISA YA KEKI HII INAUZWA GHALI SANA KWENYE MADUKA LAKINI NI RAHISI SANA KUTENGENEZA

MAHITAJI

420 gram unga wa ngano
180gram cocoa powder
1 1/2 kijiko kidogo cha chai baking soda
1 kijiko kidogo cha chai chumvi
360 gram sukari nyeupe
 2 mayai
1 kijiko kidogo cha chai  vanilla essence
360 gram maziwa ya maji
120 gram siagi
840gram caster sugar
5 gram chumvi
1 chupa ya maple syrup
1 kijiko kidogo cha chai kahawa ya unga
2 kopoza matunda ya cherry au strawbery
480 gram heavy whipping cream
1/2 kijiko kidogo cha chai vanilla esence
1 tablespoon kirschwasser
0.5 chocolate block
1 lita ya heavy whipping cream

JINSI YA KUPIKA

Washa oven iwe na 350 degrees F (175 degrees C). Weka greese proof peper kwenye chombo chako cha mviringo cha kuokea keki yako kama hauna chukua karatasi nyeupe isiyo na mistari ipake siagi yote kisha weka chini ya chombo unachookea keki yako itasaidia keki isiungue.

Kisha changanya unga wa ngano, cocoa, baking soda na 1 kijiko kidogo cha chai chumvi. Weka pembeni.

Chukua 1 lita ya heavy ceam na sukari nyeupe piga mpaka iongezeke na iwe nyepesi kama povu. Kisha weka mayai na vanilla.

Baada ya hapo mimina unga wa ngano uliokua umeuchanganya na cocoa pole pole kwenye ule mchanganyiko wa sukari na cream ukichanganya kwa kutumia mkono, mchanganyiko wako utakua mzito mimina maziwa pole pole ukichanganya kwa kutumia mwiko mpaka ichanganyike vizuri kabisa, kisha mimina kwenye vyombo vyako viwili vya kuokea keki hiyo.

Choma keki hii kwenye nyuzi joto 350 degrees F (175 degrees C) kwa dakika 35 mpaka 40, Au mpaka utakapo choma toothpick kwenye keki yako kisha itoke safi bila uji uji wa keki. Ipoze kabisa kisha toa ile karatasi kwa chini kisha kata keki yako nusu kwa mduara. Kisha nyunyizia maple syrup kwenye keki yako katika kati najuu.

Kwenye bakuli la wastani piga kwa kutumia machine au mchapo siagi mpaka iwe laini. ongezea caster sugar, 5 gram chumvi, na kahawa; piga mpaka ilainike. kama mchanganyiko wako unakua bado mzito basi ongezea vijiko 2 vya chai maziwa. Ipakaze layer ya keki na mchanganyiko huu 1/3 ya mchanganyiko. juu pakaza 1/3 ya matunda cherries ya kopo. Endelea kufanya hivyo kwa layer zilizobakia.

Katika bakuli tofauti kabisa piga tena 480 gram cream mpaka ipande na iwe kama povu kumbuka kuweka 1/2 kijiko cha chai  vanilla. Pakaza cream hiyo juu ya keki na pembeni mwa keki. Kisha rushia kwajuu chocolate curls au vipande vya chocolate ulivyokwangua kutoka kweney chocolate block. Jinsi ya kukwangu toka kwenye chocolate block tumia potato peeler.Huu ndio muonekano wa chocolate block unaweza kukwaruza kwa kutumia kisu kisha hizo chenga chenga ndio unatupia kwa juu juu na pembeni
PICHA ZAIDI JINSI YA KUIPAMBA KEKI HII NITAZIWEKA KESHO ILI KUKURAHISISHA ZAIDI WEWE MTENGENEZAJI


3 comments:

Anonymous said...

hi, naomba upost recipe ya hiyo BLACK FOREST CAKE..would appreciate it, a lot ! :-)
Thanks!!

Flora said...

Hi Chef Issa, tafadhali maelezo ya recipe hii naona hukuyaweka sawa kwa maana ya kwamba hukuelezea vizuri ni mchanganyiko gani unatakiwa uuchanganye kwenye mchanganyiko gani. Tufafanulie tafadhali ili somo liingie vizuri.
Asante.

shamim a.k.a Zeze said...

THIS IS MY FAVORITE CAKE!!