CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Friday, September 24, 2010

JIFUNZE KUTENGENEZA WALI HUU MAARUFU SANA NCHINI NIGERIA NA GHANA

WALI HUU MAARUFU SANA KAMA JOLLOFU UNALIWA SANA NIGERIA NA GHANA KAA TAYARI KWA RECIPE

MAHITAJI

240 gram ya mchele wowote ule
1 kijiko kikubwa cha chakula mafuta ya kupikia 
1 kijiko kidogo cha chai binzali nyembamba ( cumin seed)

1 kijiko kidogo cha chai unga wa binzali
1/4 kijiko kidogo cha chai unga wa kungu manga (nutmeg powder)
1 kitunguu maji kikubwa 
20 gram kitunguu swaumu
10 gram tangawizi
150 gram uyoga wowote ule
1 au 2  pili pili mbuzi mbichi (sio lazima)
1 kijiko kikubwa cha chakula nyanya ya kopo (tomato paste)
2 nyanya ya kuiva kubwa chop chop 
1 carrot kata vipande vidogo vidogo 
60 gram maharage mabichi
60 gram njegere mbichi 
10 gram chumvi
1 fungu majani ya giligilani (corrienda)


JINSI YA KUPIKA FATA MAFUNZO CHINI KAMA PICHA ZINAVYOONYESHA




Weka katika sufuria au kikaango mafuta ya kupikia kijiko 1, kishs weka cumin seeds zikisha pata moto zikapasuka weka kitunguu maji, tangawizi, kitunguu swaumu na pili pili mbuzi vyote viwe umekata chop chop na uendelee kukaanga.




Kisha ongeza carrots koroga na kisha weka chumvi.




Kisha weka tomato paste, nyanya ya kuiva uliyokata vipande vidogo pamoja na curry powder. Pika mapka uhakikishe nyanya imeiva. Kisha weka wali. Kaanga wali wako kwa dakika 3 hakikisha moto ni wa wastani.




Ksha ongeza maji 480 gram,  onja chumvi kama haitoshi ongeza tena kidogo,Kisha funika kikaango chako au sufuria na pika mpaka maji yakauke kabisa



Kisha weka maharage mabichi na njegere na uyoga hakikisha ulisha zichemsha kabla kama ni mbichi basi unatakiwa uzipike wakati unaweka mchele mwanzo kabisa ili nazo ziweze kuiva.






Hakikisha unakoroga vizuri kabisa mpaka inachanganyika saafi, kisha ongeza unga wa kungu manga pika kwa dakika 5 ili ladha ichanganyike safi kabisa kati ya wali wako na mboga majani.

 


Mwisho kabisa weka majai ya korienda ili kuongeza ladha na harufu nzuri hakikisha una mpatia mlaji chakua hiki kikiwa cha moto.

Pia badala ya uyoga unaweza tumia nyama ya ngombe au nyama ya kuku na pia hata prawns lakini inabidi uzikaange nyama hizi wakati unaweka mchele ili ziive pamoja na unatakiw aukate vipande vidogo vidogo sana iwe rahisi kuiva.

FURAHIA NA FAMILIA YAKO




3 comments:

Anonymous said...

asante sana chef,yaani now naelekea suparmaket pata hayo maitaji leo nijinome huu wali,mm nmeolewa na mkameruni huu wali nauonaga sana na naupenda,ngoja leo mie nimpikie mzee

Anonymous said...

chef nlijaribu pika hii menu kam anlivoahidi hapo juu,mambo yalikua safiii kabisa,nliambatanisha na peanut sauce yaani familia ilifurahia sana,asante sana,plz tufundishe jinsi ya kuoaka fish kama sato ktk oven,mara nyingi wangu anakuwaga mkavu sijui nakosea nn

Anonymous said...

Samahani Chief sijaelewa kidogo hapo juu huu kwenye mchanaganyiko baada ya kuweka karoti unaweka mchele au wali coz mie uwelewa wangu mchelee ni ukiwa mbichi ila wali mchele ukipikwa ukaivaa ndio unakuwa wali so hapa kwenye hili pishi letyu mchele unapikwa kwanza ndio unauchemsha au ukiwawa mbichi hivyo hivyo? asante Chief