CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Friday, October 29, 2010

JIFUNZE KUTENGENEZA SUPU YA BEETROOT


 RECIPE SAFI KABISA YA SUPU HII ADIMU YA BEETROOT, SUPU HII INAFAIDA TATU KATIKA MWILI WA BINADAMU MOJA INASAIDIA KULINDA MWILI JUU YA KUPATWA NA KANSA, PILI INASAIDIA UTENDAJI KAZI MZURI WA MAINI, TATU NI KUPUNGUZA HATARI YA CHOLESTROL KATIKA MWILI JENGA TABIA YA KUNYA SUPU HII ANGALAU MARA 1 KWA WIKI NDANI YA FAMILIA YAKO.


MAHITAJI

2 beetroot, Kisha zisafishe na uzimenye vizuri 
1 kubwa carrot
1 celery
1 kitunguu maji kikubwa
5 gram kitunguu swaumu
60 gram nyanya iliyosagwa
1 bay leaf ( sio lazima)
3 mbegu za karafuu
5 mbegu za pili pili manga
720 gram za maji baridi safi na salama
5 gram ya chumvi
90 gram maji baridi safi na salama
3 kijiko kidogo cha chai juisi ya limao


JINSI YA KUANDA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINIHuu ndio muonekano wa mboga aina ya beetroot ikiwa mmbichiKatika kikaango weka kijiko kimoja kikubwa cha mafuta ya kula kisha weka vitunguu maji kaanga mpaka vilainike (Kumbuka kukatakata vitunguu katika muonekano huo).
KIsha chukua kwaruzo au greater na ukwaruze beetroot moja, chukua 90 grama za maji baridi changanya na juisi ya limao kisha chemsha. Usiweke jikoni weka pembeni na ufunike kwa dakika 30.


Kisha kataka beetrooth, celery na carrot katika maumbo madogo madogo kama muonekano katika picha, kisha weka katika kikaango chenye vitungu na uongezee kitunguu swaumu.Kaanga kwa dakika 2 hakikisha unaweka na chumvi pia.Kisha weka ile nyanya ya kusaga na ukaange kwa dakika 2 tena. 
Ongezea mbegu za pili pili manga na mbegu za karafuu. Kisha weka maji 720 gram, Kisha pika kwa dakika 20 mpaka 30 mpaka mboga zote ziive na kua laini.
Kisha toa mfuniko na weka ile beetroot uliyokwaruza pamoja na ju, Acha ichemke kama dakika 1 tu toa mpatie mlaji ikiwa ya moto kabisa na unaweza ukapamda juu na majai yeyte yale ya kijani kuongeza utanashati.
 
 KAMA NILIVYOKUSHAURI WAPATIE FAMILIAYA YAKO ANGALAU MARA MOJA KWA WIKI SUPU HII KULINDA AFYA YA MWILI 

1 comment:

mtengera said...

walaji wengi wamekuwa si wabunifu na hata hawana haja ya kuulizauliza aina gani ya vyakula na kwa wakati gani