CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Saturday, October 2, 2010

UTAMBUE UBORA NA WASIFU WA MKATE WA BROWN


JIFUNZE JINSI YA TENGENEZA MKATE WA KAHAWIA ULIOCHANGANYWA NA MBEGU ZA UFUTA (SESAME BROWN BREAD)


MAHITAJI240 gram mbegu za ufuta ( sesame)
480 gram maji safi 
60 gram oatmeal au ( oats)
60 gram maji 
60 gram maziwa 
2 kijiko kidogo cha chai amira ya chenga 
180 gram maji safi ya uvugu vugu
30gram asali mbichi 
60 gram mafuta ya maji (vegetable oil)
3 maziwa ya unga kijiko kikubwa cha chakula
720 gram unga wa ngano 
240 gram unga wa Atta ( unga wa kahawia) 
2 kijiko kikubwa cha ufuta kwajili ya kurushia juu ya mkate 
 
JINSI YA KUANDAA FATA MAELEKEZO HAPO CHINI KATIKA PICHAChukua maji gr 480 chemsha ndani yake ufuta wa 240 gram kwa dakika 10 hadi 15,


Baada ya ufuta wako kumeza maji vizuri. Weka pembeni ipoe vizuri.


Kisha chukua 60 gram za oatmeal, 60 gram za maji na 60 gram za maziwa kisha chemsha mpaka maji na maziwa vikaukie kabisa. Kisha weka pembeni ipoe.


Chukua 180 gram ya maji ya uvugu vugu weka katika bakuli safi kisha mwagia 2 vijiko vya amira ya chenga ndani yake kisha acha ikae kwa dakika 5 tu.

Katika mchanganyiko wa maji na amira weka Asali, mafuta, maziwa ya unga kisha koroga kwa kutumia mwiko wa mbao au kijiko ili mchanganyiko wako uchanganyike vizuri. 

Kisha weka 240 gram za unga wa ngano katika mchanganyiko huo wenye amira pamoja na chumvi kishaendelea kukoroga. 


Kisha ongeza ufuta ulioupika pamoja na oatmeal kisha endelea kukoroga. Ongeza unga wa Atta 240gram pamoja na unga wa ngano 240 gram endelea kukanda.

Mchanganyiko wako ukishaanza kua mgumu, mwaga unga kidogo juu ya meza ili kusaidia mchanganyiko wako usigande hamishia hapo mchanganyiko wako na kisha endelea kukanda. (kama unatumia mashine endelea kukanda tu ).


Endelea kuongeza unga kidogo kidogo mpaka mchanganyiko wako uwe mgumu na unavutika, unatakiwa kukanda dakika 5 kwa mashine na kwa mkono ni dakika 10 hadi 15. Mchanganyiko wako lazima uwe mkavu na unavutika kiasi uweze kutengeneza miduara na iwe katika umbo safi.

Chukua bakuli safi kisha lipake mafuta ya maji na kisha weka humo ndani yake mchanganyiko wako wa mkate, Ugeuze geuze mchanganyiko wako ili uenee mafuta na kisha funika na taulo safi kwa juu ya bakuli.


Acha mchanganyiko wako katika joto la kawaida la chumba ukae kwa masaa 2 kisha utaongezeka na kuumuka kama uonavyo katika picha.


Kisha toa mchanganyiko wako na ukande kwa umbo la mviringo. Lakini unaweza kutengeneza katika umbo lolote upendalo wewe. Kisha chukua brush kama huna chukua kitambaa loanisha maji na upake juu ya mchanganyiko wako wa mkate.
Kisha nyunyizia kwa juu 2 vijiko vya ufuta mkavu. Kisha acha mkate wako uumuke tena na kua na umbo mara 2 ya mwanzo. Washa oven iwe na moto wa 400 degrees.


Oven ikishapata moto weka mkate wako ndani. Chini ya oven rushia maji kidogo ili yatengeneze mvuke utasaidia mkate wako uwe kau kau kwa juu na kutengeneza gamba gumu la kahawia choma kwa dakika 30. Kama mkate wako haujaiva funika na aluminium foil  kwa juu ya mkate kwa dakika 15 choma tena utakua umeiva. Mkate safi ulioiva ukiugonga unalia kama shimo kwa ndani.


Acha mkate wako upoe katika kopo la kuchomea kisha utoe weka pembeni upoe kabisa. Kisha unaweza kata slice au vipande vidogo na ukafurahia kwa kula na salad au soup ya moto.


Huu ni muonekano wa mkate wako ukiwa umekatwa.
Huu ni muonekano wa mkate wako safi kabisa baada ya kuiva ukiwa katika umbo la mduara unaweza tengeneza umbo la aina yeyote ile inatengenea na chombo chako cha kuokea kina umbo gani.

MKATE HUU NI MTAMU SANA SANA NA NI MAARUFU SANA DUNIA NZIMA KWA UBORA WAKE

WAPENZI WOOTE WA BLOG HII NAWATAKIA WEEKEND NJEMA3 comments:

Unknown said...

kaka Issa tupe recipe, mama yangu huu ndiyo mkate wake!!

Anonymous said...

KARIBU SANA HOME. SASA NAONA KAMA ITAKUWA USUMBUFU KWA WEWE KUWEKA NAMBA, YAKO ILA NAFIKIRI UGESENA LABDA TUKUONE WAPI MARA UTAKAPO KUWA DAR. NI USHAURI TU.

Unknown said...

Allah Bless you, lol nikirudi home inshallah nitampikia mama yangu apate kufurahia mkate huu