CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Sunday, February 21, 2010

JINSI YA KUPIKA MAPISHI MBALI MBALI YA WALI

KWA WALE NDUGU ZANGU MLIOKO UGHAIBUNI MCHELE ASILIMIA 90% HAUNA LADHA NA HARUFU NZURI KAMA TULIOUZOEA NYUMBANI CHUKUA UJANJA HUU ILI UFANYE WALI WAKO UWE WA KUNUKIA NA LADHA SAFI KABISAKaroti iliyokwaruzwa vizuri, nyanya na vitunguu vilivyokatwa katika umbo dogo dogo rahisi kwa kuiva


Mchanganyiko wa karoti, kitunguu na nyanya katika kikaango chenye mafuta na moto mkali pika kwa dakika 5 tu usiache ziive sana kisha changanya wali wako ambao umeshaiva.Huu ni wali ulioiva na ukachanyanywa na mchanyiko wako wa caroti, utapata harufu nzuri na ladha nzuri sana kwa kupata harufu na ladha nzuri zaidi unaweza ongezea pilipili hoho au girigilani ( Corriender leaves).


Mahitaji
720gram caroti iliyokwaruzwa

480gram Basmati rice ( mchele wa pishori) iliyopikwa

2 vitunguu vikubwa vikate katika size ndogo

1 Nyanya moja kubwa ikate katika size ndogo

1 fungu la majani ya girigilani

2 kijiko kikubwa cha chakula karanga zilizokaangwa kwajili ya kupambia

3 kijiko kidogo cha chai cha mafuta ya kula

Chumvi weka kulingana na ladha na mahitaji yako

Jinsi ya kuandaa:

Pasha moto sufuria lako au kikaango weka mafuta kisha weka vitunguu kaanga kiasi tu visiungue au kua na rangi ya kahawia vilainike tu inatosha.

kisha weka nyanya zikaange mpaka zichanganyike kabisa zitengeneze rojo rojo
Kisha weka caroti zilizokwaruzwa katika mchanganyiko wako kaanga na zichanganyike vizuri

Kisha weka wali wako wa basmati ulioiva katika mchanganyiko wako wa karoti changanya vizuri kisha mimina majani ya girigilani na changanya pole pole mwisho kabisa weka karanga zako ambazo zimekaangwa vizuri kama unatumia.

Mapishi haya unaweza tumia mchele wa aina yeyote ile sio lazima mchele wa basmati

4 comments:

Hilda said...

Mambo vipi chef Issa?? Naomba utuwekee pia jinsi ya kutengeneza Mikate ya kawaida (White Bread)

Hilda

Anonymous said...

khaaa!! wee kaka unapika hivi????

hii mwisho wa road

Anonymous said...

Shukran kaka Issa, maana ni headache hii michele ya huku hailiki kwa kweli, sasa kwa maarifa haya angalau tutaweza kula vizuri.

Anonymous said...

hi.....issah nimependa sana da way unavoandaaa chakula chako kinaonyesha kitamu yaani ukila hushibi