CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Thursday, February 25, 2010

JINSI YAKUTENEGEZA SHAAMI KABAB
MAHITAJI:

500 gm nyama ya ngombe

100 gm chickpeas ( )

400 gm maji

1 kitunguu kata kidogo dogo sana

4 Pili pili ya kijani mbichi

1 Tangawizi mbichi

3 mayai

3  hiliki kavu

3 (pieces cinnamon sticks) miti ya mdalasini kavu

4 karafuu

8 Mbegu za pili pili manga

1 fungu la majani ya girigilani (corienda)

1 kijiko kidogo cha chai pili pili ya unga nyekundu (red chilli powder)

 1/2 chumvi kijiko kidogo cha chai

2 lita mafuta ya kula


JINSI YA KUTENGENEZA

Loweka njegere kavu kwa masaa 24

Kisha Chemsha nyama ya ng'ombe, njegere, hiriki, karafuu, mdalasini, pilipili manga na chumvi mpaka iive na maji yaanze kukauka katika sufuria yako.

Kisha weka mchanganyiko wako katika blender saga mpaka upate mchanganyiko mzito kama tope.

Kisha changanya yai 1 tu lililopigwa vizuri katika mchanganyiko wako wa nyama uliosagwa kisha ongezea unga wa pili pili nyekundu, pili pili ya kijani, kitua nguu, majani ya girigilaninkisha changanya kwa mkono au mwiko vizuri.

Kisha weka kiaango chako katika jiko mafuta kwajili ya kukaangia yapate moto,chukua mayai mawili yaliyobakia piga vizuri weka pembeni

Chukua mchanganyiko wako wa nyama na tengeneza maumbo ya mvirngo au umbo lolote lile upendalo kisha kandamiza kwa juu upate umbo bapa ili iweze kuiva chovya katika mayai kisha tumbukiza katika mafuta ya moto kwenye kikaango. Kaanga mpaka upate rangi nzuri ya kahawia pande zote nzuri.
Kula ikiwa ya moto kwa kutumia sosi ya ukwaju na salad unaweza kula kama snack pia unaweza kula kama mlo kamili kwenye pilau au biriyani.

Inatosha kwa watu 6 mapaka 8 Furahia chakula na familia yako.
PILI PILI SIO LAZIMA PIA KAMA KUNAKIUNGO HUTUMII AU HUKIPENDI USIWEKE NA KABAB YAKO BADO ITAKUA SAFI TU.

2 comments:

Ruky said...

Asante sana ISSA leo ndio mara yangu ya kwanza kufungua blog na nimefurahi kukutana na recipe hii.napenda sana kebab ila nilikuwa sijui zinavotengenezwa. mungu akubariki

Anonymous said...

chikpeas ndio nini kaka angu kwa kiswahili?, yani im busy hapa getting the mahitaji, but hilo sijajua nini kwakiswahili