CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Thursday, October 21, 2010

JIFUNZE KUPIKA WALI WA UKWAJU


WALI HUU SI MAARUFU SANA INGAWA SIKU UKIUJARIBU UTAPENDA KUULA KILA SIKU HAHAHAHAAAAAAAA !!!!


MAHITAJI

Mahitaji kwajili ya mchuzi wa ukwaju unauwezo wa kukaa katika friji bila kuaharibika kwa miezi 2
 
200 grams za ukwaju jitaidi utoe mbegu
2 au 5  pili pili nyekundu zilizokauka
50 grams choroko
1 kijiko kidogo cha chai mbegu za mastad
240 gram mafuta ya ufuta kwajili ya kupikia (sesame oil) 
10 gram chumvi
       
    Mahitaji Kwajili ya unga 
     
    5 kijiko kikubwa cha chakula mbegu za giligilani (coriander seeds) 
    5 -10 pili pili kavu au dried red chillies (sio lazima) 

     
    Mahitaji ya wali wakati wa maandalizi
      240 gram wali uliopikwa (wali uliokwisha pikwa unapendeza zaidi hata wali uliopikwa ukalala pia unafaa)
      1 kijiko cha chai choroko
      120 gram za karanga
      120 grama za korosho
      5 majani ya binzali curry leaves 
      2 kijiko cha chai mafuta ya mawese (sesame oil)
      5 gram chumvi

        JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI





        Loweka ukwaju ndani ya maji kiasi cha 480 gram kwa muda wa nusu saa au dakika 30.




        Kumbuka ukwaju wako unatakiwa uwe hauna mbegu, kisha weka katika blenda na saga mpaka upate uzito kama uji kabisa




        Kisha chuja katika chujio ili kutoa vipande vya maganda ya ukwaju.




        Baada ya kuchuja hakikisha mchanganyiko wako ni mzito wa wastani kama ni mzito sana ongeza maji ya moto kiasi na kisha rudisha katika blenda saga na toa tena chuja na upate mchanganyiko mzito wa wastani na usiwe mwepesi sana.




        Hizi ndio mbegu za giligilani zikaushe katika kikaango tayari kwa kusaga



        Kisha ziweke katika blenda kwajili ya kusaga.




        Baaada ya kusaga na ukapata unga safi kabisa weka pembeni katika chombe kwajili yamatumizi ya wali kumbuka ukizidisha unga huu utaleta ladha ya uchungu katika wali wako.
         



        Sasa tunatengeneza mchuzi mzito. chukua kikaango weka mafuta yakishapata moto weka pili pili kavu nyekundu, mbegu za mastad na dengu au choroko



        Kisha weka ule mchuzi wa ukwaju au ( sauce!)




        Sasa tunaanza kupika pole pole. weka moto mdogo na pika kwa muda mrefu kiasi. kisha harufu ya ubichi ya ukwaju itapotea, maji yatakauka na ukwaju utakua umejipika na mafuta yatakuja juu. ngezea kijiko kimoja kidogo cha chai unga wa mbegu za giligilani kuongeza harufu safi na ladha ya kuvutia.




        Kisha toa katika moto, mchanganyiko huo wa ukwaju hifadhi katika chombo na iache ipoe. Ikipoa safi inakua tayari kwa matumizi ya wali.

        KUMBUKA
        TKiaasi cha uzito wa mchuzi wako wa ukwaju ndio ubora zaidi pia kumbuka mafuta yakiwa mengi kiasi yanasaidia kuihifadhi kwa muda mrefu, ikiwa na mafuta kiasi itaharibika mapema maana mafuta yakiwa yanaelea kwa juu yanazuia wadudu kupenya na kuozesha mchuzi wa ukwaju .
        Sasa hapa ndio tunapika wali wenyewe, 1 kijiko kidogo cha chai mafuta ya kupikia, weka dengu, kama mpenzi wa pili pili weka pamoja na majani ya binzali, kisha ongeza karanga na korosho.




        Kisha ongezea kijiko kimoja cha mafuta ya ufuta, mchuzi wa ukwaju  2 kijiko kikubwa cha chakula pamoja na chumvi, Kisha weka wali na koroga mpaka vichanganyike safi kabisa . Kisha mpatie mlaji chakula kikiwa cha moto.



        Huu ni muonekano safi wa wali huu ukiwa tayari umeshaiva na tayari kwa mlaji kufurahia




        Viungo ni viingi lakini sio kazi kuandaa chakula hiki na familia yako ikafurahia utamau wa wali huu

        ENJOY WITH YOUR FAMILY


        

        4 comments:

        Anonymous said...

        hi mbona umetoa mchoro tu bila maelekezo kam ufanyavyo katika mapishi mengine hii ni ngumu kujua jinsi ya kupika huo wali wa ukwaju

        Anonymous said...

        Umenoga looh! recipe tafadhali

        Anonymous said...

        jamani mbona umetunyima uhondo hujaweka maelezo plz tuwekee wengine tunafaidi humu humu kwenye blog

        Mama jeremiah said...

        asante kwa recipe chef Issa. Hii inabidi kuikalia hasaa. Maana naona inahitaji ufundi. Nitajaribu halafu nitakupa jibu