NIMEOMBWA NA WADAU WENGI SANA KURUDIA MAFUNZO HAYA HASA KWA WALE NDUGU ZANGU MLIOKO UGHAIBUNI MCHELE ASILIMIA 90% HAUNA LADHA NA HARUFU NZURI KAMA TULIOUZOEA NYUMBANI CHUKUA UJANJA HUU ILI UFANYE WALI WAKO UWE WA KUNUKIA NA LADHA SAFI KABISA
MAHITAJI
720gram caroti iliyokwaruzwa
480gram Basmati rice ( mchele wa pishori) iliyopikwa
2 vitunguu vikubwa vikate katika size ndogo
1 Nyanya moja kubwa ikate katika size ndogo
1 fungu la majani ya girigilani
2 kijiko kikubwa cha chakula karanga zilizokaangwa kwajili ya kupambia
3 kijiko kidogo cha chai cha mafuta ya kula
Chumvi weka kulingana na ladha na mahitaji yako
Huu ni muonekano wa caroti iliyokwaruzwa safi kabisa pamoja na nyanya na kitunguu kilichokatwa kidogo kidogo rahisi kwa kuiva
Huu ni muonekano wa wali wa maji ulioiva
Mchanganyiko wa karoti, kitunguu na nyanya katika kikaango chenye mafuta na moto mkali pika kwa dakika 5 tu usiache ziive sana kisha changanya wali wako ambao umeshaiva.
Huu ni wali ulioiva na ukachanyanywa na mchanyiko wako wa caroti, utapata harufu nzuri na ladha nzuri sana kwa kupata harufu na ladha nzuri zaidi unaweza ongezea pilipili hoho au girigilani ( Corriender leaves).
Jinsi ya kuandaa
Pasha moto sufuria lako au kikaango weka mafuta kisha weka vitunguu kaanga kiasi tu visiungue au kua na rangi ya kahawia vilainike tu inatosha.
kisha weka nyanya zikaange mpaka zichanganyike kabisa zitengeneze rojo rojo
Kisha weka caroti zilizokwaruzwa katika mchanganyiko wako kaanga na zichanganyike vizuri
Kisha weka wali wako wa basmati ulioiva katika mchanganyiko wako wa karoti changanya vizuri kisha mimina majani ya girigilani na changanya pole pole mwisho kabisa weka karanga zako ambazo zimekaangwa vizuri kama unatumia.
Mapishi haya unaweza tumia mchele wa aina yeyote ile sio lazima mchele wa basmati
6 comments:
kweli ile ladha ya Mbeya si mchezo.
Asante chef
Asante sana Chef Issa.
Mungu azidi kuwabariki!
aisee nilipika pia hiki chakula
zamani nilikua nachanganya pamoja na kuiva pamoja,haikunoga kama sasa nilipopika wali pekee na nikakaanga mchanganyiko baadae
delicious!!
real delicious, nilipika bwana nyumba nzima walijitafuna vidole,
asante cheff.
baba wawili
nakwenda kuupika kesho kwenye Eid, naimani wageni wnagu wataenjoy
Post a Comment