CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Monday, June 21, 2010

WAPENZI WA SPAGHETI, NYAMA YA NG'OMBE NA SAUSAGE KAAENI TAYARI KWA RECIPE

CHAKULA HIKI NI KIZURI SANA KWA WAPENZI WA SOSEJI NA NYAMA PIA

MAHITAJI

5 soseji zilizoiva tayari
1 kilo fillet ya nyama ya ng'ombe
1 fungu la majani ya korriender
 200 gram uyoga wakopo au fresh sawa tu
100 gram karoti
100 gram pili pili hoho
500 gram za nyanya pika mchuzi wa nyanya saafi mzito kisha weka asali ya nyuki vijiko viwili  cha chakula pamoja na limao 1 kamulia na soya sosi kijiko 1 cha chakula.


Huu ni muonekano wa soseji iliyoivwa na ikakatwa upande wa kushoto, katikati ni nyama ya ngombe iliyochemshwa ikaiva nayo imekatwa nyembembea kwa urefu kama inavyoonekana katika picha na mwisho upande wa kulia ni mkati mwembamba wa karoti, pilipili hoho na uyoga wa kopo.


Huu ni muonekano wa paketi 2 spagheti zilizo chemshwa tayari kwa kuchanganywa na nyama


Huu ni muonekano safi wa mchuzi mzito uliochanganywa na soya sosi, limao na asali


Chukua  mchanganyiko wote wa nyama, soseji na uyoga ulio na mboga kisha kaanga kwenye kikaango pamoja na majani ya korienda ( Giligilani) kwa dakika 2 tu


KIsha weka spagheti iliyochemshwa ndani ya mchanganyiko wa nyama kaanga kwa dakika 1 tu kisha mwagia ndani mchuzi wa nyanya saafi na endelea kuchanganya mpaka mchanganyiko wako wote uwe na mchuzi na unaladha safi ya mchuzi wa nyanya.


Kisha pakua weka katika sahani kwa mtindo wa mlima kama unavyoona kwenye picha kisha mwagia tena majani kisai ya korienda kwa juu ya chakula hiki. Unaweza kula na cheese kwa juu pia inaongeza ladha safi ya chakula choko. Chakula hiki kinauwezo wa kuliwa na watu wa 5 na wakashiba na kufurahi kabisa.

FURAHI ANA FAMILIA YAKO KWA CHAKULA HIKI SAFI2 comments:

Anonymous said...

tunasubiri kwa hamu kaka hiyo recipe tuzidi kuongeza upendo majumbani mwetu. tupe vituuuuuu!!!!

Anonymous said...

lini sas utaandaa hiyo maana danasubiria kwa hamu sana