CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Sunday, March 14, 2010

CHAPATI NA NYAMA YA MBUZI

Chakula hiki ni rahisi sana kupika hata mabachela wanaweza kula safi bila kutumia muda mwingi jikoni na mama kama umechelewa kurudi nyumbani watoto na baba wanataka kula chakula hiki kinashibisha ni rahisi kuiva na nikitamua familia itafurahi sana sana.
Kata mboga aina nne kama inavyoonyesha katika picha kitunguu maji, karoti na pili pili hoho kisha ziweke vizuri pembeni
Pika chapati zako saafi kusha zikate kwa umbo la pembe tatu na zipange kwenye sahani kama inavyoonekana katika picha.
Kisha weka nyanya na mboga majani aina yeyote ile uipendayo wewe katika picha nimeweka karoti na zucchini ya kuchoma.
Kisha chukua nyama ya mbuzi ulioikata vipande vidogo vidogo kama ulivyokata mboga zako kisha weka mafuta kwenye kikaango kisha ipate moto mkali sana weka nyama ya mbuzi kaanga mapaka ikauke maji iliyotoa kisha weka mchanganyiko wa mboga zote kaanga kwa dakia 2 kisha weka nyanya ya kopo kiasi na maji kidogo upate mchuzi mzito  toa kwenye kikaango na weka katika sahani kula bado ikiwa ya moto ohhhh safi san hiii.2 comments:

Anonymous said...

Mara nyingi nimekuwa nikipika maini kama hivi, sasa nitapika Mbuzi.

Asante sana kaka.disminder.

Anonymous said...

Ah we kaka issa umeoa? haki ya nani nataka mume wa aina yako. Niwe napikiwa mapocho pocho.