CHICKEN COMFY NI CHAKULA SAFI SANA PIA KINASAIDIA SANA KATIKA UCHUMI WA NYUMBANI KUMBUKA FAMILIA ZETU ZA KIAFRIKA NI KUBWA KUKU MMOJA UNALISHA WATU 10 HADI 12 NA KILA MTU ANAFURAHIA NA KURIDHIKA.
MAHITAJI
500gram karoti
300gram kitunguu
500 gram pili pili hoho
150 gram mafuta ya kupikia
1/2 kijiko kidogo cha chai chumvi
25 gram kitunguu swaumu
1.5 kilo kuku
JINSI YA KUANDAA FATA MAELEZO KATIKA PICHA
MAHITAJI
500gram karoti
300gram kitunguu
500 gram pili pili hoho
150 gram mafuta ya kupikia
1/2 kijiko kidogo cha chai chumvi
25 gram kitunguu swaumu
1.5 kilo kuku
JINSI YA KUANDAA FATA MAELEZO KATIKA PICHA
Chukua kuku mmoja mzima mwenye kilo moja na nusu kisha mchemshe katika maji na chumvi aive kabisa nyam iwe laini.
Kisha inyofoe nyofoe hiyo nyama kakitka kuku mifupa weka pembeni kumbuka kutoa mifiupa yote kwa umakini zaidi ni hatari kwa mlaji. Baada ya kuinyofoa nyama na kuitenganisha na mifupa utabakia na gram 800 au 700 gram.
Huu ni ni muonekano wa jisi ya kuzikata mboga kisha zichanganye zote kwa pamoja katika kikaango zikaange ziive tu kiasi. kisha weka kitunguu swaumu na changanya ile kuku ulionyofoa na kua na mfano wa mikato kama ya kuku pika kwa dakia 2 au 3 katika kikaango ni kiasi cha mboga na kuku kuchanganyika na ile kuku ipate tu moto.
Kisha weka katika sahani inaweza kuliwa na wali, ugali, viazi au chapati. Chakula hiki ni salama hata mtoto anaweza kula maana hakina mfupa na mchanganyiko huu wa mboga unaleta ladha safi sana.
Chakula hiki unaweza kulisha watu 10 na kila mmoja anakua amekula wastani wa gram 200 za mchanganyiko wa mboga na kuku inatosha kabisa iwe ni hotelini au nyumbani. Pia kumbuka kula na mchuzi wa nyanya au mchuzi wowote ule upendao.
5 comments:
great.. my friend from Tanzania ( Omari ) tell me about your blog. And now i am looking your blog, really very well. And my english isn't good i am soryy:)
ps.:i am from Turkiye, my friend Omari is here for his education.
Tunasubiri kwa hamu
Hi Chef Issa? Asante kwa kutupatia darasa ila nilikuwa naomba nikurudishe nyuma kidogo, kule kwenye mapishi ya biskuti za karanga, nilitaka kujua unatumia karanga mbichi zilizotwangwa au zilizokaangwa na baadae zikatwangwa. Nitashukuru kupata ufafanuzi zaidi.
Asante sana kaka.
Kwa familia zetu bongo, hapa umesema. Kila mtu atakula kuku na kufurahi.
disminder.
Hi chef Issa, hongera kwa kwa kazi nzuri, unajua kutengeneza Röst, hebu tujuze natumaini upo uswiss, mimi nipo hapa Luzerne, huwa napenda sana hicho chakula ila nikiwa bongo nashindwa tengeneza huwa nanuna iliopo tayari coop, naajua ni viazi vinakunakunya je huwa vinachemsha kabla au je unaweka nini na nini.
Post a Comment