CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Tuesday, March 2, 2010

WAPENZI WA SALADI SALAMA KWA AFYA


SALAD HIZI HULIWA KABLA YA MLO KAMILI KAMA KITANGULIZI


Chemsha spinach au mchicha uive nusu tu kisha weka pembeni upoe

Kata vitunguu vidogo kwa urefu

Changanya mafuta ya maindi ili isaide ukiweka katika friji salad yako isigande

weka chumvi kulingana na ladha yako

weka maji ya limao au vinega ksiah changanya pamoja tayari kwa kula panga kama inavyoo onekana katika

piachasalad hii ni asfi na salama kwa afya yako



SALD YA VIAZI NA MICHIRIZI YA SOSEJI ZA NG'OMBE


Upande wa kulia mwanzo ni michirizi ya soseji, jani la saladi na mwisho ni mchanganyiko wa viazi vilivyochemshwa vikaiva nusu vimechanganya na mayonaise kidogo na pili pili hoho na kitunguu kilichokatwa kidogo kidogo.




Kwanza weka jani lako la salad kisha weka mchanganyiko wa viazi juu ya jani la salad hakikisha inakaa katika umbo la mlima ili kuvutia zaidi




Mwisho kabisa weka vipande vya nyanya freshi na kati kati weka michirizi ya soseji muhudumie mlaji ikiwa ya baridi 


KUMBUKA KUWEKA MAYONAISE KIDOGO SANA KWA AFYA YAKO




7 comments:

Anonymous said...

asante sana chef,maana unatufanya waume zetu wawahi kurudi kwa msosi wa nyumbani...hahaha ila nilikua na swali na hizi salad ni muda gani muafaka wa kuliwa?ni kabla ama baada ya mlo mkuu?ama ni wakati wowote?

Julia.

Anonymous said...

Jinsi ninavyopenda mapishi? Sijui nimepatwa na nini? Asante kaka, majibu utapata.

disminder.

Anonymous said...

leo ni mara yangu ya kwanza kufungua blog yako ni nzuri sana na inaelimisha kupita kiasi. Naomba unifundishe aina mbalimbali za utengenezaji wa salads za kula baada ya mlo au pamoja na mlo

JJ said...

kaaazi kwelikweli,tushindwe wenyewe,maana mwalimu ameamua kutufundisha bure bila gharama yoyote,keep it up chef maana kwa jinsi navyopenda kupika..............

Anonymous said...

Jamani mimi ninachokuombea ni Mungu akuzidishie zaidi na zaidi uwe na moyo huo huo wa kutoa mafunzo bila malipo. Kwa upande wangu nimefaidika sana.

Anonymous said...

Hallow chef nimefurahi sana kupata mapishi kama haya nakushukuru sana na mungu akubariki sana Mungu akulinde na magonjwa.

Sarah, Arusha

Sarah said...

asante sana chef mimi napenda sana kupika nimefurahi sana na mapishi yako Mungu akulinde akuzidishie pale palipopungua asante