CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Thursday, March 4, 2010

SOMO LA KUPANGA CHAKULA SAFI CHA KIAFRIKA KATIKA SAHANI LINAENDELEA

SAMAKI WA NAZI

Jinsi ya kupika na kuandaa samaki wa nazi mtamu kuliko wote hahahahahahahaaa!!!!



Weka wali na mboga zilizochomwa kiasi zikaiva nusu wala hazijaungua kama unavyoona katika picha



Kisha chukua kipande chako cha samaki kibichi kipakae kitunguu swaumu na tangawizi iliyosagwa ikachanganywa na maji ya limao, chumvi na mafuta ya kupikia kidogo acha kwa nusu saa ndani ya mchanganyiko huo.

Kisha kipake unga wa ngano kidogo na kiweke kwenye kikaango chenye mafuta kidogo sana kaanga kwa moto wa wastani hadi aive ukitaka kujua samaki kaiva choma na toothpick akitoa maji hajaiva asipotoa maji kaiva Kisha muweke katika sahani kama picha inavyoonyesha.




Kisha andaa mchuzi wako wa nyanya uliotiwa tui zito la nazi mimina juu ya samaki na kuachia kipande kidogo bila mchuzi ili kumuonyesha mlaji kua huyu ni samaki mkavu



Huu ndio muonekano halisi wa samaki wako furahia na familia yako kwa kufanya mabadiliko ya mezani


MSHIKAKI WA SAMAKI AINA YA KING FISH



Maboga ni chakuka safi sana pia unaweza kula yakichanganywa na viazi ulaya. Pika boga lako pamoja na kiazi ulayampaka kiive kabisa kisha kipondeponde na kupata mchanganyiko safi kabisa.

Weka katika mchanganyiko wako kitunguu kilichokatwa kidogo sana na pili pili manga pamoja na chumvi na krimu kidogo au maziwa kicha changanya vizuri upate mchanganyiko mzito weka huo mchanganyiko wako katikati ya sahani kisha panga mboga. juu yake weka mshikaki wa samaki na mbele yake weka mchuzi wowote ule utakao penda kulia samaki wako.

Hotelini mgeni atafiurahia sana na nyumbani familia itafurahi kupita maelezo.


NYAMA YENYE ROJO SAFII


Nyama safi iliyo[ikwa kwa mchuzi mzito yaweza kua ni ya ng'ombe au mbuzi au kondoo weka wali wako safi pembeni kisha choma mboga aina nne nyanya, kitunguu, bilinganya na karoti kisha zipange kama inavyoonekana katika picha.


2 comments:

Ruky said...

Chakula kinaonekana kitamu kwenye sahani, asante sana kwa mafunzo

Anonymous said...

Mambo!

Yaani kaka najuuuuta kukufahamu maana napenda sana kupika na nilikuwa sijapata shule ya mapishi bloguni ikaniingia kama hii.uko juu!
Sasa nakuomba utuandalie pia ratiba ya chakula kwa wk yaani kuanzia asbh mpk dinner maana huwa tuna kuwa na kazi wengine mpk unamwambia msichana leo pika chochote sasa kukiwa na karatiba aaah hata dada unamwambia soma humu na hata ukirudi unakuwa na hamu ya chakula na zaidi hujui kilichopikwa basi utaenjoy tuu.

Mdau wako mgeni kabisa,

Mama P!