CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Sunday, March 7, 2010

JINSI YAKUTENGENEZA SALAD YA MCHANGANYIKO WA MBOGA

Mahitaji basamic vinagrate

60 gram balsamic vinega
2 sukari ya kahawia kijiko kidogo cha chai

1 kitunguu swaumu cha kusagwa kijiko kidogo cha chai
½ chumvi kijiko kidogo cha chai
½ pili pili manga ya unga kijiko kiodogo cha chai
180 gram olive oil

Jinsi ya kuandaa balsamic ninegrate

Weka katika bakuli balsamic vinegrate, sukari, chumvi, pili pili manga na kitunguu swaumu changanya mpaka sukari iyeyuke.

kisha mimina mafuta ya olive kidogo kidogo huku ukichanganya na mchapo mpaka mafuata yote umimine kisha itakua tayari kwa matumizi ya salad yako.

Inasaidia kuongeza ladha katika mboga zako na
Salad hii  ni safi kwa afya ya mlaji, inamchanganyiko wa nyanya, matango, karoti, pili pili hoho na zucchin ya kukwaruzwa ikachanganywa na limao, mafuta ya mahindi na chumvi.Panga nyanya zako kama inavyoonekana katika picha


Kisha panga matango yaliokatwa kwa mduara


Kisha weka kariti upande wa kuliaKisha weka pili pili hoho upande wa kushoto


Finyanga kwa mkono ile salad ya zucchini iliyokwaruzwaKisha iweke mbele ya sahani kati kati ya nyanyaKisha chukua balsamic vinagrate mwagia juu ya matango yako pole poleHuu ndio muonekano wa salad yako yenye mchanganyiko safi wa mboga unaweza kula kabla ya chakula au baada ya chakula safi kabisa ni rahisi kutengeneza na aihitaji muda mwingi wa kuandaa na muonekano na ladha ni safi kabisa.


 
4 comments:

ruky said...

Si mchezo! nimebaki namshangaa huyo bata kwa dk kadhaa

Anonymous said...

mbona salad yenyewe kiduuchuuu!!!

Lulu said...

Yaani hata sijui nikushuru vipi Chef kwa mambo yako, yaani mi kila weekend ni kupika misosi toka kwa recipe zako. thank you. Nitakutumia picha za mapishi yangu nami

Anonymous said...

yaani chef unatisha,swali langu balsamic vinega ndio ipi hiyo???