CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Saturday, March 27, 2010

REDWINE CABBAGE, BBQ FISH NA PUMPKIN

WAJUA BOGA LINAPENDEZA SANA UKILA NA KABECHI ILIYOPIKWA NA MVINYO MWEKUNDU PAMOJA NA MSHIKAKI WA SAMAKI?
Menya vizuri boga na ulikate katika muonekano wa umbo zuri kama inavyoonekana katika picha. Lichemshe mapak liive ila lisibondeke kumbuka libaki na umbo lake zuri ili lipendeze katika sahani
Kisha weka kabechi yako katika sahani nyuma ya hilo boga.

Jinsi ya kuipika hiyo kabechi kwanza kata kata kabechi katika mkato mdogo mdogo kisha iweke kwenye maji na mvinyo mwekundu ( red wine) iwe ya kutosha ichemshe kwa masaa 4 mapak kabechi yote ibadilike rangi iwe nyekundu kumbuka pombe yote huyeyuka wakati unapika kitakachobaki ni harufu nzuri ya zabibu zilizosindikwa.kisha panga mboga ziliizochomwa pembeni ya boga na kabechi
Unaweza pia kuipamba kwa stail hii weka kabechi chini kisha weka boga kwa juu kisha unafata mshikaki kumbuka maji yale yanayobakia wakati unachemsha kabechi yatumia kama sauce pembeni ya kulia boga na mshikaki wako safi wa samaki.


Kumbuka wakati unachemsha pombe yote inayeyuka hakuna kilevi chochiote kinachobakia chakula hiki ni salama hata mtoto anawezakula na akafurahia kabisa.

Jinsi ya kutengeneza mshikaki wa samaki angalia katika blog achieve utaona jinsi ya kuandaa BBQ party kisha fungua angalia jinsi ya kutengeneza aina tofauti za mishikaki.

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante kwa mpiko huu ni chakula changu ambacho nakipenda sana nitatengeneza.

Anonymous said...

mmh thanks naomba utupe malezo ya kuandaa hiyo red wine cabbage!!
asante kwa mada zako za chakula

Anonymous said...

sasa Redwine kwa wale tusiyekunywa pombe si tatizo.