CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Thursday, April 1, 2010

BEEF SATAY MHHH YAM YAM YAM !!!

SATAY SAUCE UNAWEZA KUTUMIA KATIKA AINA YEYOTE YA NYAMA NA INALADHA KUBWA YA KARANGA

MAHIAJI
70 gram mafuta ya kupikia
150 gram kitunguu maji chop chop
1kilo Nyama ya ngombe au mbuzi au samaki au kuku
200 gram Soya sauce
500 gram karanga iliyosagwa ya kopo
pili pili ya unga au tabasco au pilipili fresh ( weka kulingana na ladha unayoweza kula)
500 gram maziwa ya maji
1 kijiko kidogo cha chai unga wa mdalasini
300 gram Nyanya ya kopo
1/2 kijiko kidogo cha chai pili pili manga
1/2 kijiko kidogo cha chai unga wa kayene
1 kijiko kidogo cha chai kitunguu swaumu kilichosagwa
1 kijiko kidogo cha tangawizi iliyosagwa
300 gram maji
100 gram vinega au maji ya limao.

JINSI YA KUANDAA

Weka mafuta katika sufuria kisha weka kitunguu maji, kitunguu swaumu, tangawizi, unga wa cayene, unga wa mdalasini, pili pili manga kaanga vichanganyike vizuri kwa dakika 2 -3

Kisha weka  nyanya ya kopo changanya vizuri, kisha weka karanga ya kusagwa changanya mpaka ichanganyike vizuri. kisha weka maziwa ya maji pamoja na maji koroga mpaka upate mchanganyiko safi kabisa mziti kama haijakorogeka vizuri tumia mchapo wa chuma.

kisha weka pili pili fresh au pili pili ya unga na juice ya limao. acha ichemke kama ni nzito sana ongeza maji au maziwa mpaka upate mchanganyiko mzito wastani na kama imekua maji sana basi ongeza karanga ili iwe nzito.


Kata nyama vizuri iwe katika umbo jembamba kama muonekano katika picha na iweke kwenye miti ya mishikaki ichome kwenye griller au jiko la mkaa yote sawa mpaka iive kabisa.



Hii ndio muonekano safi kabisa wa sauce nzito ya karanga ni tamu sana na unaweza kuitunza kwa miezi 2 - 3 katika freezer bila kuharibika ukawa unatumia kidogo kidogo kumbuka kuigawa katika kiasi kidogo utachokua unatumia ili kila unapohitaji usiyeyushe yote unapoyeyusha na kugandisha tena unaruhusu wadudu kuingiua na sauce yako itaharibika.



Kama kawaida weka wali au ugali au chips katika sahani kwa muonekano thabiti na mzuri ili kumvutia mlaji. Kwa mtummoja mpatie mishikaki mitatu ya nyama hahahahahahaaaaaa ikiwezekana muongeze maana ni mitamu sana sana.



Mwagia sauce juu ya nyama pole pole saafi kabisa. Kumbuka sauce yako isiwe maji iwe nzito ili iweze kushika katika nyama na ndio inabeba ladha nzima ya chakula.



Huu ni muonekano safi kabisa wa chakula hiki kizuri naimani familia yako itakipenda sana na watakusifia mama kila unapoingia jikoni basi watoto watakua wanakuja kukusumbua kwa harufu nzuri wanaona kama chakula kinachelewa.

KAMA HAUNA KARANGA YA KUSAGWA BASI KAANGA KARANGA KISHA ZIPIKE HIVYOHIVYO KWA KUFUATA UTARATIBU KAMA ILIVYOELEKEZWA BAADA YA KUIVA CHUKUA BLENDER SAGA UTAPATA SAUCE SAFI NA LADHA NZURI SANA.




2 comments:

Ruky said...

wow hiki chakula kinaonekana kitamu sana nitajaribu kupika wk end hii

Unknown said...

Hii nimeikubali kaka, umenikumbusha sana kwa bibi.