BISKUTI ZA MHOGO
MAHITAJI:
Unga wa mhogo Vikombe 2
Sukari Robo kikombe
Mafuta( Margarine) Nusu kikombe
Yai Moja
Amira Kijiko cha chai 1
Karanga zilizosagwa Moja kikombe.
NJIA YA KUTAYARISHA:
1. Changanya unga wa mhogo, sukari, mafuta na amira pamoja mpaka vyote vichanganyike vizuri
2. Ongeza yai na karanga kisha changanya mpaka mchanyiko umekuwa laini.
3. Sukuma kwenye ubao ulinyunyiziwa unga kisha kata umbile la biskuti kwa kutumia kikombe.
4. Weka matundu ya kutolea hewa kwa uma au kijiti
5. Weka kwenye chombo cha kuokea kilichopakwa mafuta. Oka kwa muda upatao dakika kumi mpaka biskuti imekuwa na rangi ya kahawia hafifu.
Huu ndio muonekano wa biscuti ya unga wa muhogo pia unaweza changanya ladha kwa kuongezea karanga au korosho zilizokaushwa au kukaangwa pia unaweza weka zabibu kavu.
KAMA HUTUMII SUKARI PIA UNAWEZA KUTUMIA ASALI IDADI SANA NA SUKARI NA BISKUTI ZAKO ZITAKUA NA LADHA SAFI SANA
MFULULIZO WA MAFUNZO YA UNGA WA MUHOGO YANALETWA KWENU NA HAJAT ASIA KAPANDE
1 comment:
Asante sana Cheff Issa na Hajat Asia Kipande.
Inamaana kama nitatumia Asali badala ya sukari au nitatumia sukari ile ya diabetic biskuti hizi mama yangu anaweza kula?
Nasema asali kwa sababu nimezowea kutumia katika cake nimpikiazo mama yangu. Ila cake yake inataka ufundii inakuwa lainiiiiiiiiiii
kazi njema
Post a Comment