UNGA WA MUHOGO UNAWEZA UKABADILISHA KABISA LADHA NA AINA YA MAPISHI NYUMBANI KWAKO KWA UPANDE WA VITAFUNWA KWAJILI YA CHAI ASUBUHI AU CHAI YA JIONI HATA KATIKA SHEREHE NDOGO ZA MAJUMBANI KWETU KILA SIKU NITAKUA NAWAWEKEA RECIPE YA CHAKULA KIMOJA KIMOJA
RECIPE HIZI ZA UNGA WA MIHOGO ZINALETWA KWENU NA MWALIMU WANGU ALIYENIFUNDISHA JINSI YA KUANDAA CHAKULA TOKA NIKIWA MDOGO KABISA MPAKA LEO NIMEKUA CHEF KAMILI YEYE NI FOOD AND NUTRITION SPECIALIST MAMA YANGU MZAZI ASIA KAPANDE
RECIPE HIZI ZA UNGA WA MIHOGO ZINALETWA KWENU NA MWALIMU WANGU ALIYENIFUNDISHA JINSI YA KUANDAA CHAKULA TOKA NIKIWA MDOGO KABISA MPAKA LEO NIMEKUA CHEF KAMILI YEYE NI FOOD AND NUTRITION SPECIALIST MAMA YANGU MZAZI ASIA KAPANDE
Mama yangu mzazi Hajati Asia Kapande akiwa Egypt anaelezea bidhaa na matumizi bora ya via zilishe
KEKI YA MIHOGO
MAHITAJI:
Unga wa mhogo Vikombe vitatu
Sukari ¾ kikombe
Mafuta (Margarine) Kikombe kimoja
Amira ya unga Vijiko vya chai vitatu
Mayai Matatu.
NJIA YA KUTAYARISHA
1. Koroga sukari na mafuta pamoja mpaka mchanganyiko uwe laini na mwepesi
2. Piga mayai mpaka yawe mepesi.
3. Chekecha unga na amira pamoja
4. Ongeza unga na mayai taratibu kwenye mchanganyiko wa mafuta na sukari.
5. Mchanganyiko ukiwa mzito ongeza maziwa kidogo au maji. Endelea kuongeza unga na mayai kidogo kidogo mpaka unga wote umekwisha.
6. Ongeza chenga za ganda la limao kidogo ( linaongeza ladha).
7. Paka mafuta chombo cha kuokea kisha weka mchanganyiko wa keki kwa ujazo wa ⅔
8. Oka kwenye jiko lenye moto wa wastani kwa muda upatao dk. 20 au mpaka keki imeiva vizuri.
1 comment:
Habari za masiku kaka, kabla hata ya blog haijaanza matangazo via 8020 fashion na michuzi mpaka inaanza sikufahamu ka ni wewe, Duh kitu cha ajabu leo ndo siku nimegundua kumbe ni mwenyeji wa Nyegezi Kilimo Hivi sasa sauti/malimbe. Enzi zile za Nyamalango p/school. yaani nakupa big up saaana..... Ni msomaji mzuri mana mimi ni hotelier by professional. Vipi unakumbuka mawese, mapera, machungwa na zambarau ya kule nyumbani? Big up sana tena sanaaaa.
Post a Comment