CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Tuesday, April 20, 2010

JE UNAIJUA POTATO ROSTII

HII NDIO POTATO ROSTII NI CHAKULA MAARUFU SANA KWA WASWISS

MAHITAJI

4 Viazi vikubwa
50 gram siagi
10 gram chumvi
5 gram pilipili manga ya unga

Chukua viazi vimenye maganda kisha viweke katika maji baridi na vichemshe kwa dakika 15 - 20 kisha vitoe vitakua vimeiva ingawa vitakua vigumu kumbuka visiwe laini au visiive sana viweke pembeni vipoe.






Kisha chukua kwaruzo la caroti ( greater) vikwaruze viazi upate vipande vidogovidogo safi na vigumu



baada ya hapo changanya chumvi na pili pili manga



kisha weka siagi katika kikaango chenye leya nyeusi inayosaidia chakula kisiungue na kunga'nga'nia katika kikaango kinaitwa ( non stick pan) weka ujazo wa kikaango kidogo au kama ni kwa chakula cha watoto tumia chombo cha kukatia umbo la aina yeyote ile utakayopenda kisha weka viazi ndani ya umbo hilo kaanga upande wa kwanza kisha kaanga upande wa pili kuwe na rangi ya kahawia safi.





Rostii potato itakua tayari na utafurahia chakula chako pia unaweza kwaruza viazi hivyo na ukahifadhi katika freezer hata kwa miezi miwili na visiharibike kumbuka uwe tu umeviweka katika saizi unayopenda kupika kwa baadae usiviache vitawanyike lazima uwe umevitengeneza katika umbo.

Kama utakua umevitengeneza katika umbo lolote lile na ukaviweka katika freezer ukivitoa unaweza kuvipika kwa mitindo tofauti kabisa unaweza ukavioka katika oven au uka vikaanga kwenye mafuta mengi maana vinakua vimeshikana.

FURAHIA CHAKULA HIKI NA FAMILIA YAKO.


2 comments:

Anonymous said...

kaka ile menu ya watoto vipi?

Anonymous said...

haloo Isa ´nakuaminia wangu, nilikuomba utuwekee, haya tupe mambo naisubiriii kwa hamu,asante kwa kujali.