CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Saturday, April 3, 2010

HIVI NDIO VYAKULA KWAJILI YA PASAKA

PATA MAELEKEZO JINSI YA KUANDAA KUANZIA SUPU, SALAD, MAIN COURSE MAPAKA DESSERT KWAJILI YA PASAKASalad ya viazi ulaya, maharage mabichi, kipande cha nyanya, tunda la olive na vipande vya cheddah cheese

Chemsha viazi ulaya visiive sana na maharage mabichi pia chemsha yasiive sana kisha acha yapoe.
chukua viazi na maharage changanya na chumvi kidogo na mafuta ya mahindi kisha weka katika sahani kama inavyoonekana mwagia kidogo balsamic vinega chora mistari miwili kama inavyoonekana katika picha. Mwisho weka juu vipande vya chizi na tunda la olive.Hii ni classic Italian minestrone soup

100 gram Njegere
1/4 paketi spagheti au noodles
100gram grcarrot
100 gram kitunguu
100 gram leeks
100 gram grzucchini
100 gram cabbage
200 gram Nyanya ya kopo
pili pili manga na chumvi

chukua mafuta ya siagi 150 gram weka katika jiko kisha kaanga mchanganiko wote wa mboga hizo kwa dakika 3 tu kisha nyanya ya kopo kaanga kiasi kisha weka maji wastani mpaka mboga zote zizame katika amji kisha weka spagheti au noodles na chemsha mpaka ziive zikishaiva weka chumvi na pili pilimanga kwa mbali kisha hudumia supu yako ikiw aya moto pia unawez hifadhi katika friji kwa siku 7 hadi mwezi katika freezer kwa matumizi ya baadae.Hii ni nyama ya sungura na mint sauce

Chukua mguu wa sungura chemsha katika maji na chumvi, kitunguu swaumu na pilipili manga kwa muda wa saa 2nyama itaiva vizuri na kua laini sana.

Toa nyama hiyo kata kata weka katikasahani na kisha chukua mint sauce inauzwa madukani weka lile rojo zito kwenye maji chemsha kwa dakika 5 sauce hiyo itakua safi sana weka juu ya nyama ya sungura au nyama ya kondoo kula na wali na ugali pia.hii ni chicke pyramid ohhh ni ngumu kiasi kutengeneza soon nitaweka picha 10 zinazoonyesha mtiririko jinsi ya kuiandaa ila ni tamu sana na inaliwa na njegre za nazi na pilau kama unavyoona katika picha.
Hii ni honey grazed ham

Kwanza kabisa chukua roll nzima ya ham ichemshe kwa masaa 2 kisha kata slice ya honey grazed ham kisha weka slice ya nanasi, kisha weka slice za bacon ya nguruwe na juu yake weka slice za nyanya na mwisho kabisa weka slice za cheddah cheese. mwisho chemsha kiasi red wine katika kikaango kwa dakika 2 tu halafu mwagia pembeni ya chakula hiki.

Unakula na potato wheels na grilled vegetable kama inavyoonyesha katika picha kumbuka kuhudumia ikiwa yamoto.Hii ni oven backed apple with cinamon sugar and vanila sauce

chukua apple kisha likate slice halafu chukua unga wa ngano na mayai piga pamoja kisha chukua slice za apple weka katika lile rojo la unga chova kisha toa panga hizo apple katika bakinga tray mwagia mafuta kiasi kisha zichome kwa moto wa watani zikisha badilika rangi zitoe.

kumbuka unatakiwa uwe umeshaandaa cinamona sugar( sukari ya mdarasini) ukitoa tu yale ma apple kwenye oven chovya katika hiyo sukari na kumbuka kuhudimia mlaji apple zikiwa bado zamoto.
Hii ni Calamerized cream na ladies finger biscuit, cherry na zabibu

Chukua sukari yeyote ile weka katika kikaango mpaka iungue iwe ya kahawia kisha weka maziwa changanya haraka haraka mpka upate rojo zito kisaha iache ipoe.

Chukua cream fresh tumia mchapo chapa mpaka iwe nzito kabisa iwe kama povu kama unamashine tumia kuchapa kwa urahisi zaidi kisha chukua lile rojo la sukari iliyopoa tumia kijiko kuchnagnaya cream iliyokma povu na lile rojo la sukari ya kahawia kisha weka katika chombo kizuri au bakuli dogo pamba na bikuti kama hapo juu na zabibu au strawberry.

FURAHIA PASAKA NA FAMILIA YAKO KWA CHAKULA NAFUU NA RAHISI KUTENGENEZA.


3 comments:

Anonymous said...

bro we ni mkali man big up sana

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante sana! Pasakla njema kakangu!

Anonymous said...

shukurani, nangoja kwa hamu hayo maelekezo, Inshaallah nitavipika..asante sana