MAHITAJI
1 kilo Nyama yeyote ile iwe kuku, mbuzi au ngombe
300 gram nyanya ya kopo au fresh ila katakata iwe ndogo ndogo kwa mchuzi
50 gram kitunguu swaumu
100 gram karoti
100 gram kitunguu maji
100 gram pili pili hoho
1 paketi la macaroni
300 gram viazi ulaya
JINSI YA KUANDAA FATILIA CHINI KATIKA PICHA
Huu ni muonekano wa nyama ya mbuzi naipenda sana
Weka kitunguu kwenye kwenye mafuta ya moto kisha kaanza mpaka kiwe na rangi ya kahawia
Kisha weka kiuongoa aina ya paprika kuongeza ladha kama hauna usiweke
kisha weka nyama kaanga pai mpka iive kumbuka kuweka maji kikombe kimoja kidogo kusaidia isiungue
huu ndio muonekano wa macaroni
Baada ya nyama kuiva weka viazi ulaya vibichi kaanga pia mpaka viive
kisha weka unga wa binzali kuongeza ladha
Kisha weka kitunguu swaumu kuongeza ladha na harufu safi pia na kukata harufu ya nyama ya mbuzi
Kisha weka karoti na pili pili hoho pamoja na nyama ya kopo
Weka makaroni kwenye maji moto yaliyokiwsha chemka sana chemsha kwa dakika 7 tu
weka chumvi kwenye makaroni yaliyopo jikoni wakati yakiendelea kuchemka
Baada ya makaroni kuchemka toa weka katika bakuli kisha yapoze ma maji baridi sana ili yasipondeke
Kisha chuja vizuri makaroni yako wasiwe na maji na chukua nyama yako ya mcuzi iliyokweisha iva changanya na makaroni yako yaliyoiva pia koroga ya changanyike vizuri
Kisha weka makaroni yako kwenye bakuli la kioo au la chuma ili uyaoke kwemye oven mchuzi ule ushikane safi na macaroni yako kua na muonekano na ladha safi
Kisha weka katika oven na oka kwa dakika 10 kumbuka kuweka aluminium foil kwa juu ili yasiungue
BAADA YA DAKIKA 10 MACARONI YAKO YATAKUA SAFI NA TAYARI KWA KULIWA WAPAKULIE FAMILIA YAKO YAKIWA YA MOTO KUMBUKA KUWEKA USAWA MACARONI , KIAZI NA NYAMA USIWEKE MAKARONI TUPU HAHAHAAAAAAAA
8 comments:
Uwiiiiiiiiii, watu people, yaani umenigusa kama niko ITALY VILE. CANT WAIT
im waiting in vain for the macaron recipe chef plz post!
jamani hata mimi nangoja sana recipe ya macaroni halafu naomba utupostie recipe ya biriani plzzzz chef
chef umepotelea wapi tena?
nasubiri kwa hamu kaka hiyo recipe ya macaron. lete vitu.
mambo chef,naoma unijuze kuhusu hiyo paprika,naitumia kwa nyama zote au?ni nini na inatumikaje?naomba jibu..halaf napata wapi hivo viungo unavotumia?
mungu akubariki uendelee kutupa mambo mazuri kama haya
Asante sana kaka. mimi mpenzi wa makaroni umenifikisha
kaka unatisha yaani mi binafsi nakukubali sana,nadhani mkeo atakuwa anafaidi sana.endelea kutupa maujuzi kaka na sisi tufanye maajabu kama yako.ahsante mrs.D
Post a Comment