CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Monday, March 8, 2010

CHAKULA KILE KILE SAFI CHA KIAFRIKA UKIKIPANGA SAFI KITAPENDEZA SANA


UGALI, KUKU WA NAZI NA KACHUMBARI


Muonekano wa picha ni safi na ladha ya chakula ni nzuri kupita maelezo kata ugali wako safi kisha weka katika chombo cheny umbo lolote zuri upendalo kisha weka katika sahani.

Chukua jani la salad weka kachumbari na mwisho pakua vipande vya kuku vilivyopikwa katika mchuzi mzito wa nazi.

JINSI YA KUTENGENEZA KUKU WA NAZI

Chuku kuku wako uliekisha mkata vipande, chkua kitunguu swaumu na kitunguu maji weka na mafuta ya kupikia katika blender saga upate mchanganyiko kisha mwagia kwenye kuku wako acha kwa nusu saa mchanganyiko huo uingie katika nyama

Chukua nyama ya kuku weka kwenye sufuria bila maji kuku huyu atajichuja maji na kuchemka, chemsha kwa dakika 30 tu kwa moto wa kawaida kisha toa kabla maji hayajakauka.

Kisha kata kitunguu na nyanya

Weka mafuta katika sufuria, kisha weka kitunguu kaanga kilainike kisiungue, kisha weka nyanya  ya kopo kidogo koroga kiasi na baadae weka nyanya fresh koroga mapaka iive safi kabisa.

Kisha weka wake kuku wako wakavu bila mchuzi waliokwishachemshwa koroga mpaka nyama ishikane safi na mchuzi wako wa nyanya kisha weka ule mchuzi uliobaki wakati unachemshia kuku ili kutunza ladha halisi ya kuku wako.

Ikishachemka kwa muda chukua tui la nazi kama ni ya unga au fresh weka katika mboga yako ya kuku na pika kwa moto wa wastani mpaka mchuzi upungue na kua mzito.

Onja chumvi na kuku wako atakua tayari kuliwa


POTATO BRAVAS


Kwa wale wapenzi wa chakula cha wala mboga Majani ( Vegetarian) hiki ni chakula safi sana.

Chukua viazi kata katika maumbo ya pembe nne au dice au mkato wowote ule ilimradi viwe vidogo rahisi kutafuna kwa mlaji. Kisha chemsha kwa dakika 10 tu vitoe viweke katika oven oka kwa dakika 25 kisha vitakua vimeiva na kukauka vizuri.

Toa weka katika sahani kisha miminia mchuzi mzito wa nyanya ( mchuzi wa nyanya liotengenezwa kwa nyanya na vitunguu ukawa mzito ruksa kuongeza kiuongo chochote kulingana na ladha unayopenda wewe)juu yake na vitunguu vilivyokaangwa kiasi vitaleta harufu nzuri na ladha safi mwisho pamba na jani la parsley.

Kula kama mlo kamili mchana au usiku furahia na familia yako.
8 comments:

Anonymous said...

kwanza kabisa, hongera chef kwa ushindi wako. pili naomba uteleze jinsi ya kutengeneza chocolate, kama umeweza kushina uswiss basi choc zako zitakuwa bomba!!!!!
mdao

Anonymous said...

Asante kaka nakufagilia sana.

disminder.

Anonymous said...

Hongera sana kaka,ila ningependa kujua ni jinsi gani ya kutengeneza kuku wa nazi?maana napenda sana kuku ya nazi.
Tania

Anonymous said...

Unaposema mchuzi wa nyanya una maana ya nyanya pekee?

Anonymous said...

Mambo Chef Issa. Naomba utupe funzo la mapishi ya pudding.

Asante.

Ruky said...

nimeipenda hii potato bravas, simple and health, thank you

Anonymous said...

Hongera sna chef samahni naona maelekezo ya kupika kuku wa karanga asante sna nitashukuru kwa msaada wako!

Anonymous said...

nimepika leo hii potatoe bravas ni bomba si mchezo...yaani umenifundisha kupika kitu rahisi na haraka....shukrani sana