CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Thursday, March 11, 2010

JINSI YA KUTENGENEZA CREAM CARAMEL

MAHITAJI

300 gram fresh cream
1.5 gram maziwa ya maji
700 gram sukari
1 chupa ndogo ya vanilla essence
16 mayai 

Caramel hii ni kwa watu 27

FATA MAELEKEZO JINSI YA KUTENGENEZA HAPO CHINI KAM PICHA ZINAVYOELEKEZA




Andaa vifaa vyako utakavyotumia mayai, maziwa, cream, vanilla ya maji na sukari



Muonekano katika picha ni vyombo utakavyotumia kuchomea caramel yako unawez tumia chombo chenye umbo lolote kinachoweza kuhimili joto la kwenye oven


weka maziwa lita 1 kwenye sufuria pamoja na cram 300 gram ili kuongeza ladha safi na ubora wa caramel yako iwe laini na tamu hahahahaaaaa!


Weka vanilla chupa nzima ndogo ndani ya mchanganyiko wako wa maziwa na cream ili kuuwa harufu ya mayai baada ya kuiva



Weka sukari 300 gram ndani ya mchanganyiko wako wa maziwa na cream



Kisha pembeni chukua bakuli kubwa vunja mayai 16 yachape kiasi ute mweupe na wanajo vichanganyike kisha weka maziwa yaklio bakia nusu lita changaya na mchapo yachanganyike kisha chukua ule mchanganyko wa maziwa na cream ukiwa na uvuguvugu mimina kwenye mchnganyiko wa mayai na maziwa kisha changanya ichanganyike usichape sana kiasi tu




Kisha weka sukari kwenye  kikaango ay sufuri iyeyushe mpaka iwe na rangi ya kahawia au udhurungi ( Brown)




Baada ya kuiunguza sukari weka katika chombo chako utakachotumia kuchomea karamel yako unaweza kutumia chombo chochote kile kumbuka kiwe kikavu kabla ya kuweka sukari hiyo baada ya kumimina iache ipoe kabisa



Huu ndio muonekano wa mchanganyiko mzima wa sukari, maziwa, cream, vanilla ya maji na mayai


Kisha chota na ujaze kwenye vyombo yako vya kuchomea hakikisha usijae kabisa acha nafasi kiasi baada ya hapo kumbuka kuweka maji baridi katika chombo unachotumia kuweka vyombo vidogo vyemchanganyiko wa caramel yako maji baridi yanasaidia kuchemka na kuipika pole pole kisha weka tray yako katika oven


huu ni muonekano wa karamel yako ikwa imeshaiva na unaona maji yanatakiwa kuwekwa nusu ya chombo ili yasiingie ndani ya chombo chenye mchanganyiko wa caramel



Choma kwenye oven kwa muda wa dakika 50 kwenye joto 350 degree F kama oven yako inamoto sana choma kwa dakika 15 hadi 20 tu kumbuka kuchungulia uone kama imeshaiva na kutoa rangi nzuri ya kahawia kwa juu


Baada ya kuiweka katika joto la chumba ikapoa iweke kwenye fridge iwe baridi wakati wa kula tumia kisu kuzungusha pembeni mwa chombo chako ili iweze toka kiurahisi



Leo nimekula hii dessert laini yabaridi na tamu sana sana!!



Muonekano wa cream caramel ikiwa imeishaiva imepoa tayari kwa kuliwa

KULA NA FAMILIA YAKO DESSERT HII BAADA YA CHAKULA NI TAMU LAINI NA INZVUTIA MDOMONI

Mahitaji kwaajili ya familia ukitaka kutengeneza cream caramel kidogo unawezakuitunza kwenye friji na inauwezo wa kukaa siku 7 bila kuharibika haikai kwenye friza.

Mahitaji kwa watu 5

300 gram Maziwa
 50 gram cream
2 mayai
1/4 vanilla ya maji
50gram sukari ya kuweka katika maziwa
100 gram sukari ya kuunguza

Jinsi ya kutengeneza fata maelekezo kama juu inavyoelekeza ulichopunguza ni vipimo tu

Dada Ruky naimani utakua umenielewa nashukuru sana kwa swali lako zuri.



3 comments:

Ruky said...

Asante, swali langu ni hili kama nataka kutengeza kidogo I mean ya familia ya watu wawili vipimo vinakuwaje? halafu ukiiweka kwenye friji inaweza kukuaa more than a week? au ina last kwa muda gani? na hatuigandishi?, asante

Anonymous said...

slm! naomba nikuulize nimeona ile sukari ulounguza imeweka chini na ukaweka huo urojo juu sasa je mbona naona tena sukari nyengine juu au unaweka kotekote?? dahhh napenda hiyo kitu kazi njema!!!

Anonymous said...

Jide umeona hii?
Ulitaka kujua inatengenezwa vipi.

disminder.