CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Saturday, March 6, 2010

JINSI YA KUTENGENEZA PIZA


Piza hii ni ya mboga mboga na cheese

MAHITAJI

1 kilo unga wa ngano

240 gram maji ya vugu vugu

2 olive oil kijiko kikubwa cha chakula

2 Asali kijiko kidogo cha chai

1 chumvi kijiko kidogo cha chai

1 Amira ya chenga kijiko kidogo cha


Jinsi ya kutengeneza
Chukua bakuli weka maji ya uvugu vugu, amira ya chenga, asali na chumvi kisha koroga ichanganyike vizuri acha itulie kwa dakika 10.

Kisha chukua olive oil na unga wa ngao mimina kidogo kidogo changanya mpaka ichanganyike safi kabisa kisha anza kukanda kama mchanganyiko wa chapati au maandazi.

Baada ya mchanganyiko wako kua mgumu safi kabisa funika bakuli lako na mfuko wa plastiki au cling film kwa muda wa saa 1 katika joto la chumba na mchanganyiko wako utaumuka baada ya muda huo. kisha ukandamize mchanganyiko huo wa unga na kua flati kama mwanzo.

Kama unataka kutumia kesho funika vizuri na weka katika friji. Kama unatumia leo fata maelezo katika picha hapo chini.




Huu ndio muonekano wa mchanganyiko wako wa unga tayari kwa kuandaa kitako cha piza



Kata mafungu matano hadi saba ya ujazo sawa inategemea na ukubwa wa piza unaopenda we mlaji kisha sukuma umbo la duara



Muonekano wa umbo la duara



Tengeneza mchuzi mzito wa nyanya kisha weka juu ya kitako cha piza kama inavyoonekana katika picha usisahau kuweka chumvi na sukari kidogo katika mchuzi wa nyanya ili kukata uchachu.



Huu ni mkato wa mboga mbichi nyanya, kitunguu, pili pili hoho, na bilinganya kwajili ya piza yako



Baada ya kuweka mchuzi wa nyanya weka juu mboga aina zote kwa mpangilio kama inavyoonekana katika picha



Kisha chukua mozarella cheese ikwaruze katika mkato mdogo rahisi kuyeyuka tumia kwaruzo la karoti linafaa



kisha chukua mkwaruzo wa mozarella cheese mwagia juu ya hizo mboga kama inavyoonekana katika picha



Sasa piza yako ipo tayari kuchomwa weka kwenye sahani ya bati ili isaidie kuiva upande wa chini pia  oven ambayo imeshawashwa na ina joto 400 - 450 F choma kwa dakika 20 hadi 25 iwe kaukau na rangi ya kahawia pia cheese itakua imyeyuka na kusambaa vizuri juu ya pizaa





Huu ndio muonekano wa piza yako baada ya kuiva unaweza weka mchanganyiko wa nyama yeyote ile kama salami, nyama ya ngombe, nyama ya kuku au samaki kwa kufata maelekezo sawa sawa na hii piza ya mboga  tofauti yake itakua huweki mboga unaweka nyama.



3 comments:

pretty lady said...

Ahsante kwa hili pishi la pizza, mie ni mpenzi sana wa pizza na huwa napika mwenyewe. Ila mie huwa natanguliza tomato sauce and then naweka cheese baada ya cheese ndio naweka hizo topping.

Anonymous said...

THANK YOU SANA. Ila naomba uliza "mozarella cheese" ndo ipi na pa kuipata wapi? thanks.

Anonymous said...

Thanks chef kwa recipe zako nzuri

@ 11:54 Homemade mozarella cheese hii hapa http://homecooking.about.com/od/cheeserecipes/r/bldairy22.htm
ila sijajaribu kuitengeneza mwenyewe. Nitatafuta hivi vitu halafu nitajaribu kutengeza nitakweleza ilikuaje. Sijui kama maduka ya bongo mitaani zinauzwa hizi. nakumbuka zamani tulikua tunanunua cheese kule masaki au labda mpaka mlimani city.

Na mimi pizza napenda na marinara sauce badala ya pizza sauce.

Na pia kama unatengeneza homemade pizza sauce ni muhimu ukiweka kijiko cha chai cha cornstarch au unga wangano. Inaisaidia kuifanya iwe nzito zaidi.

HTH