CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Tuesday, April 20, 2010

HII NDIO SHEPHED PIE

KIHISTORIA CHAKULA HIKI KINALIWA SANA NA WAINGEREZA

MAHITAJI

Mchuzi mzito wa nyama ya kusaga ( Bolognese)

200 gram nyama ya kusaga
50 gram kitunguu chopchop
50 gram caroti
150 gram nyanya ya kopo
50 gram pili pili hoho chop chop
50 gram mafuta ya kupikia
5 gram pili pili manga ya unga

Jinsi ya kuandaa

Weka mafuta katika kikaango kisha weka nyama ya kusaga kaanga mpaka iive kabisa kisha weka kitunguu maji, karoti na pili pili hoho kaanga kwa dakika 3 tu kisha weka nyanya ya kopo koroga vizuri kwa dakika 3 zingine weka na chumvi na pili pili manga kwa mbali mchuzi wako utakua umeshaiva.

Huu ndio mchuzi wa nyama ya kusaga

KISHA ANDAA VIAZI VYA KUSAGA

MAHITAJI
300 gram viazi ulaya
100 gram maziwa ya maji
10 gram chumvi

Chemsha viazi katika maji mpaka viive kabisa kisha vitoe na uviponde ponde kama picha inavyoonyesha hapo chiki kisha weka chumvi na maziwa koroga mpaka upate mchanganyiko laini kabisa. 



Hii ndio mush potato au viazi ulaya vya kusaga

KIsha chukua bakuli yako safi inayoweza kutumika kupikia kwenye oven weka mchuzi wa nyama ya kusaga nusu ya bakuli kisha weka juu yake hivyo viazi vyakusaga unaweza weka kawaida au ukatumia mfukowa kurembea ( Piping bag) ukapa mapambo mazuri kwa juu kama picha hapo chini inavyooonekana viazi vina mvuto. Ukimaliza weka chedah cheese kiasi kwa juu.



hii ndio piping bag unaweka viazvi vyako vya kuponda ndani yake kisha unapambia juu ya huo mchuzi wa nyama ya kusaga ukimaliza unaweka katika oven kwa dakika chache tu upate rangi nzuri ya kahawia na cheese iweze kuyeyuka.



Ni nyama ng'ombe yakusaga na viazi vya kuponda safi sana kwa mtoto pia mtu mzima



2 comments:

Anonymous said...

Lovely, my baby will love this

Anonymous said...

Bw. Chef naomba nikusahihishe kidogo hapa. Shepherd's pie nijuavyo mimi inatengenezwa kwa kutumia nyama ya kusaga ya kondoo, whereas Cottage pie ni nyama ya ng'ombe iliyosagwa in other words minced meat.

Mpenda mapishi
London