CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Friday, April 16, 2010

JE HUPENDI KULA MBOGA MAJANI? HII UTAIPENDA SANA TU!!


HATA KAMA WEWE SIO VEGETARIAN MBOGA MAJANI NI MUHIMU SANA KWA AFYA YAKO NA HASA ZIKIANDALIWA VIZURI.

Mahitaji

1 nyanya frsh ya kuiva safi
1 kitunguu
1 zucchini au baby marrow
1 pili pili hoho
1 kiazi kitamu
1 carrot
150 gram njegere mbichi
100 grm mtindi halisi usio na ladha ya matunda
150 gram Maharage mabichi

Jinsi ya kuandaa

1- Chemsha njegere kisja maharage mabichi kwa dakika 4 katika maji na chumvi yaliyochemka hasa ziive safi zisiwe na rangi ya njao zibaki na rangi znuri ya kijani
2- Chemsha kiazi kiive vizzuri ndani ya maji na chumvi
3 - Kata nusu kitungu, slice ya karoti, Nyanya, zucchini na pili pili hoho chona kwenye kikaango cheney mafuta kiasi kwa dakika 10 tu ziive ziwe na rangi ya kahawia wastani zisiungue.

kisha panga kama inavyoonekana katka picha usisahau mtindi weka kwenye bakuli dogo kwa pembeni na kiazi kikate slice na panga saafi njegere weka katika bakuli pia.

CHAKULA HIKI NI KIZURI NA UTAKUA UMEUWEKA MWILI AKO KATIKA HALI NZURI KIAFYA KWA KUZINGATI AMAPISHI BORA YA MBOGA


5 comments:

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

ni mchanganyiko gani huo?

Naona baadhi ya vitu

Ruky said...

Kaka msaada plse unga wa kayene ni nini? umeandika kwenye ile beef satay

Anonymous said...

Habari bro. nakupongeza sana kwa darasa unalotupa hapa mungu akubariki. nina tatizo moja kwenye kupika keki soft ya kula nyumbani au kama hizi za birthday na harusi sijui huwa nakosea wapi maana huwa haitoki kama hizi tunazonunua kwenye masupermarket au tunazokula kwenye masherehe ya harusi na birthday.plse bro naomba msaada -vipimo , maandalizi na steps za upish.thankx

Ruky said...

Chef nakukumbushia swali langu hapa

Anonymous said...

maziwa mgando hayo,mie nafikiria ni kama yale ya MARA meupe...