CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Thursday, April 29, 2010

WAJUA KUWAPIKA PRAWNS

BBQ PRWANS WITH GREEN CURRY SAUCE

Mahitaji

½ kilo prawns
50 gram kitunguu swaumu
100 gram maji ya limao
15 gram chumvi
50 gram prawns masala
20 gram pili pili manga

Kumbuka kuwamenya pwans na kuwasfisha vizuri

Chukua vitu vyote hivyo kwa pamoja changanya kisha weka katika friji kwa nusu saa ili viungo viingie safi katika prawns wako.


Hawa ndio prawns baada ya kusafishwa na kuwekewa viungo vyote safi kabisa


Hapa prawns wapo katika pan wanachomwa pia unaweza tumia kikaango au ukawaqchemsha kwa dakika 10 wankua wameshaiva


Huu ni muonekano wa green curry

Mahitaji

2 majani ya mchai chai
50 gram kitungu swaumu
30 gram binzali ya unga
20 gram mdalasini ya unga
20 gram binzali nyembamba ya unga
100 gram tui zito la nazi
50 gram kitunguu maji
40 gram mafuta ya kupikia
200 gram maji safi ya baridi

weka mafuta katika kikaango kisha weka kitunguu maji na kitunguu swaumu kaanga kiasi kisha weka viungo vyote vilivyobakia kaanga kidogo viive kisha weka majani ya mchai chai na maji acha ichemke kwa dakika 15 hadi 20 kisha weka tui la nazi na kama maji yamepungua basi ongezea kiasi acha ichemke tena kiasi kisha




Huundio muonekano wa prawns baada ya kuiva unaweza kuwachoma katika kkaango au ukawachemsha katika maji lakini kumbuka katika maji weka limao na chumvi ili kulinda ladha. Unaweza kula kwa viazi vya kuponda, wali au ugali


Mwisho kabisa kumbuka kumpatia mlaji na kipande cha limao kama urembo juu ya chakula pia inasaidia kuongezaz ladha kwa chakula chochote cha samaki



 

5 comments:

Anonymous said...

Nimefurahi sana leo umegusia mapishi ya prawns manake nilikuwa nikitamani sana kujua jinsi ya kuwapika.

Jayjo

Unknown said...

mmmh kaka hapa utafunga ukurusa, tupe hizo hints. Prawns jamani hatari tupu

Unknown said...

tupe kaka, mume wangu atafurahi sana, anavyopenda prawsn! uuuh

Anonymous said...

my precious delicious food prawns

kitu kizuri sana hiki,me uwa nawanunua na kuwapika mwenyewe siku zote.wanapatikana kwa uzuri pale soko la samaki kigamboni.ata nikiwa mkoani lazima niwaagizie

lol

Anonymous said...

my chef issa

ukisema gram wengine wala hatuelewi pliz labda waweza wekea kwa njia ya kijiko ivi vingapi

maana gram si mpaka ninunue vile vikombe vya kupimia?

tuwekee pia kwa njia ya kupimia kwa kijiko ni rahisi

PIA TUNGA KIJITABU/VIJARIDA VYENYE MAPISHI YAKO YOTE TUWEZE NUNUA,serious naitaji sana